Na Shushu Joel, Bukombe
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Geita Ndugu Manjale Magambo ametajwa kuwa ni chanzo cha muunganiko wa Vijana katika Mkoa huo.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Uvccm Wilaya ya Bukombe Ndg Nelvin Salabaga alipokuwa akifunga Makambi ya umoja wa vijana kata ya Bulangwa Wilayani humo.
Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa ambapo alishindwa kufika kutokana na .wingiliano wa majukumu Mwakilishi huyo wa Mwenyekiti wa Mkoa Ndugu Majale alisema kuwa kwa kweli Jumuiya imekuwa na muunganiko mkubwa kutokana na uwezo na dhamira aliyonayo Mwenyekiti Manjale
"Mkoa wa Geita umekuwa na Wenyeviti wengi waliopita katika Jumuiya yetu lakini Ndugu Manjale amezidi kuwa kiongozi wa pekee na Mwenye uchu mkubwa wa kuona jumuiya inazidi kupaa kutoka ilipo na inasonga mbele" Alisema Mwenyekiti Nelvin Salabaga
Kwa upande wake Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo ya Uvccm kata ya Bulangwa Juma Masanja alisema kuwa mafunzo haya ya siku 5 yamewajengea uwezo mkubwa wa kukifahamu Chama Cha Mapinduzi na kanuni zake jambo ambalo linakwenda kuwaongezea vijana uelewa mkubwa ndani ya chama.
Aidha amemuomba Mwakilishi wa Mwenyekiti Manjale kuendeleza mafunzo hayo kwa vijana ili Chama cha Mapinduzi kiweze kuendelea kuwa na hazina kubwa ya vijana wenye kukitambua Chama na jumuiya zake.
Naye Mwenyekiti wa Uvccm kata ya Bulangwa Ndugu Alex Marcel amewapongeza washiriki wote waliojitokeza na kuwataka kuzingatia mafunzo waliyoyapata kambini pia mafunzo hayo yakawe chachu ya maendeleo kwao na familia zao.
Aidha amemsifu mgeni rasmi kwa hotuba safi iliyojaa mafunzo na maelekezo kwa vijana .
MWISHO

0 Comments