Na Shushu Joel ,Chalinze.
WANANCHI wa kata ya Pera Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wamempongeza Diwani wa kata hiyo Ndugu Jackson Mkango kwa jinsi ambavyo amekuwa kiongozi mwenye uchu mkubwa wa maendeleo ya kata hiyo.
Akizungumza na HABARI MPYA MEDIA Mmoja wa wakazi wa kata hiyo Ndugu Hamis Maulid alisema kuwa kata ya Pera ilikuwa na changamoto lukuki za maendeleo lakini tangu Mhe Mkango ashike kijiti maendeleo yamekuwa yakimiminika kila kukicha.
Aliongeza kuwa ni vyema viongozi kama kina Mkango wakawa wanapewa maua yao wakiwa hai hii ni kutokana na jinsi ambavyo wamekuwa watu wa kusema na kutenda katika jamii wanayoiongoza.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Ndugu Jackson Mkango akizungumza kwa njia ya simu alisema kuwa maendeleo yeyote katika jamii yanakuja kwa ushirikiano hivyo ushirikiano alionao na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Ridhiwani Kikwete umekuwa chanzo cha mafanikio ya kata yetu.
Aidha Mkango amezidi kumpongeza Mbunge kwa jinsi ambavyo amekuwa hapati usingizi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Pera na Chalinze kwa ujumla kwani Pera imepata miradi mingi jambo ambalo limeondoa changamoto za wananchi kwa haraka.
MWISHO

0 Comments