Na Shushu Joel, Kibaha
BIRTHDAY ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekuja na neema kubwa kwa watanzania kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Nishati safi kwa nchi za Afrika.
Akizungumza na Wanawake wa Mkoa wa Pwani katika zoezi la kula keki na watoto wanaoishi katika kituo cha Nyumbani Hajat Mariam Ulega alisema kuwa ni vyema ni mmoja wetu kuwa champion wa matumizi ya Nishari Safi ili kuweza kuishi ndoto za Rais wetu Dkt Samia.
"Uwezo mkubwa unaoonyeshwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kielelezo tosha kuwa ni kiongozi mwenye maono makubwa na watanzania" Alisema Hajat Mariam Ulega.
Aidha Hajat Mariam Ulega aliongeza kuwa ni vyema kila mwana Pwani kuhakikisha anamuunga Mkono Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Taifa (UWT) Mkoa wa Pwani Zainab Vullu amempongeza Mbaraza kwa ushiriki wake katika shughuli za kijamii pia amewasifu viongozi wengine kwa moyo walionao.
Mwisho

0 Comments