Na Shushu Joel, Kibaha
MJUMBE wa Baraza kuu na kamati ya Utekelezaji Umoja wa Wanawake Taifa (UWT) Hajat Mariam Ulega amewaasa Wanawake wa wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kuendelea kudumisha Umoja na Upendo ndani na nje ya Jumuiya hiyo.
![]() |
| Hajat Mariam Ulega Mbaraza Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza kuu Uwt Taifa akizungumza na Wanawake wa Kibaha katika Baraza la kikanuni( Na Shushu Joel) |
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akifunga baraza la umoja huo ambapo amewakumbusha Wanawake ni jeshi linalotegemewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hivyo ni vyema tukawa na muunganiko wa pamoja.
Aidha Hajat Mariam Ulega aliongeza kuwa kuelekea uchaguzi Mkuu ni vyema kila mmoja wetu akawa balozi wa kuendelea kuyasema yanayozidi kufanywa na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Selina Koka ambaye ni mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha Mjini amempongeza Hajat Mariam Ulega kwa moyo wake wa kujitoa kwenye Chama na jamii kwa ujumla .
Pia amewataka wanawake kuendelea kushikamana kwani kipindi hiki mambo mengi yanaweza kujitokeza ya baadhi ya watu kutaka kuwatenganisha.
MWISHO


0 Comments