"DKT SAMIA SULUHU HASSAN ANA IMANI KUBWA NA WANAWAKE " M/KITI UWT BUKOMBE


Na Shushu Joel, Bukombe 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Bi, Julieth Simon amewaeleza wanawake wa Wilaya hiyo kuwa Mwenyekiti wa Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ana imani kubwa nasi.


Haya ameeleza alipokuwa akizungumza na viongozi wa UWT kutoka kata 17 za Jimbo hilo  kwenye Baraza.


Bi, Julieth alisema kuwa ni vyema watanzania wakatambua jinsi Rais Dkt Samia anavyowatendea haki watanzania kwa kushusha maendeleo makubwa kwa watanzania wote jambo ambalo limewashangaza watu mbalimbali kwa utendaji wake.


Aidha alisema kuwa ni vyema wanawake kote nchini tukaendelea kuunga mkono juhudi hizo zinazofanywa na kiongozi wetu .


Naye Mgeni rasmi katika baraza hilo ambaye ni katibu wa Uwt Mkoa wa Geita Pili Ndimila amewapongeza wanawake wa wilaya ya Bukombe kwa jinsi walivyo na umoja katika utendaji wa kazi za jumuiya .


Pia amewataka kuendelea kutoa hamasa kwa Wanawake wengine ambao bado hawajajiunga katika jumuiya ili waweze kujiunga na kupata nafasi ya kuendelea kuyasema yale yanayofanya na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan. 


Aidha amewakumbusha kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu hivyo ni vyema kujiandaa mapema kutoa hamasa kwa jamii ili kila mmoja aweze kumpigia kura kipenzi cha Watanzania Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments