Na Shushu Joel, Kibaha
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Mhe Slivesty Koka amewataka Wanawake wa Wilaya hiyo kuwapinga watu wanaokuja na kuwataka kuwafitinisha .
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Taifa (UWT) Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani katika baraza la kikanuni lililofanyika katika ukumbi wa Valentine Hotel.
Mhe Koka alisema kuwa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani kuna mbinu nyingi ambazo utumika na baadhi ya wanasiasa ambao wana nia mbaya na maendeleo ya wanakibaha hivyo watu hao ni vyema wakapuuzwa.
"Kibaha ya juzi, Jana na Leo kuna mabadiliko makubwa sana yamefanyika na hii yote ni kutokana na ujabali unaofanywa na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusukuma maendeleo kwa nchi" Alisema Koka.
Aidha amewataka wanawake wa kibaha kuendelea kutembea kifua mbele kutokana na miradi mikubwa inayofanywa na na Rais Dkt Samia kwa ushirikiano mkubwa wa Mbunge.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bi, Elina Mgonja amempongeza Mbunge Mhe Koka kwa kasi kubwa ya maendeleo yanayofanyika ndani ya kibaha huku akimtaka kuendelea kupiga kazi kwani yeye ndiye mbunge mwenye uchu wa maendeleo ya wanakibaha.
Aidha amewataka wanawake kuendelea kushikamana na kuachwa kuyumbishwa na baadhi ya watu wasio itakia mema kibaha yetu.
MWISHO


0 Comments