"AMANI TULIYONAYO TUSIICHEZEE" DKT KIKWETE


Na Shushu Joel, Bukombe 


RAIS Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mstaafu  Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewataka watanzania kuendelea kuitunza amani tuliyonayo nchini.



Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wana Chama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita katika Mkutano maalum wa usomaji wa utekelezaji wa ilani kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Mbunge wa Jimbo hilo. 


"Lazima kila Mtanzania aendelee kuwa mlinzi wa amani tuliyonayo ili Taifa letu liweze kuwa na umoja,upendo na mshikamano tuliachiwa na waasisi wa Taifa letu" Alisema Dkt Kikwete 


Aidha Dkt Kikwete amemponveza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibadilisha Tanzania katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo. 


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko amempongeza Rais Mstaafu Dkt Kikwete kwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za Mkutano maalum wa Jimbo  la Bukombe. 



Aidha amewataka wananchi wa Bukombe kuendelea kumsemea Rais Dkt Samia kwa yale ambayo  ametufanyia wana Bukombe katika sekta mbalimbali. 


"Tutampa heshima kubwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wakati ukifika yeye pamoja na mgombea mwenza wake Dkt Nchimbi ili waendelee kutuletea maendeleo" Alisema Dkt Biteko 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments