Na Shushu Joel, Rufiji
MJUMBE wa Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Taifa ( UWT) na Mbaraza wa Jumuiya hiyo Hajat Mariam Ulega amefufua ndoto za Binti Zaynabu Mkwanye ambaye alishindwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa kukosa mahitaji ya shuleni.
Akizungumza mara baada ya kumkabidhi vifaa vya shule Hajat Mariam Ulega alisema kuwa licha ya kuwa kiongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi yeye ni Mama kama walivyo Mama wengine hivyo mara baada ya kusikia changamoto za Binti hiyo ilimbidi akatishe ziara yake ili kutatua changamoto za Binti huyo.
"Binti yetu Zaynabu amepata madaftali yote ,Viatu,Sare za shule na mahitaji yote muhimu ili aweze kuanza shule kama alivyoeleza" Alisema Hajat Mariam Ulega
Aidha amewaomba watanzania kuendelea kujitolea kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa watoto wenye uhitaji ili nao waweze kutimiza ndoto zao walizonazo .
Kwa upande wake Zaynabu Mkwanye amempongeza Hajat Mariam Ulega kwa moyo wake wa kujitoa kwa watoto na wakubwa hakika huyu ni kiongozi wa kuigwa na jamii na kwa moyo huu alionao Mungu atamfikisha mbali
Aidha amesema kuwa kwa misaada hii aliyopata anakwenda kuanza shule mara moja na atakuwa mwanafunzi wa kuigwa hasa kusimulia yale aliyofanyiwa na Hajat Mariam Ulega ya kumfanya aweze KUTABASAMU kurejea shuleni.
MWISHO
0 Comments