"VIONGOZI ONYESHENI UPENDO KWA WATOTO YATIMA" M/KITI WAZAZI TEMEKE


Na Shushu Joel, Temeke


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam Ndugu Khamis Slim amewataka viongozi wa Vyama na serikali kuweza kujijengea tabia ya kuwatembelea watoto yatima na wale wenye mahitaji maalum na kuwajulia hali.


Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao kwenye hafla fupi ya Iftari iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo chini ya Mwenyekiti Slim.


Aidha aliongeza kuwa wazazi tunapopata nafasi ya kuwatembea watoto hao wamekuwa wakifarijika sana kutokana na hali halisi ya maisha yao wanayoyapitia hapa duniani.


"Watoto hawa wamekuwa wakikosa faraja zetu wazazi kutokana na mfumo wetu wa maisha hivyo ni vyema viongozi tukawa mstali wa mbele katika Jambo la kuwatembelea watoto yatima na wale wenye mahitaji maalum ili tuwe faraja kwao" Alisema Mwenyekiti Slim


Mara baada ya tukio la Iftari watoto hao wamemfanyia Dua maalum Mwenyekiti huyo kwa kile alichokifanya kwa watoto hao ili Mungu aendelee kumpa kwa pale alipotoa .


Kwa upande Ivon Msita mmoja wa walezi wa watoto hao amempongeza Mwenyekiti wa Wazazi Ndugu Slim kwa moyo wake wa upendo kwa jamii.

Aidha ameongoza kuwa viongozi kama Slim ni wa kuigwa kwenye Taifa letu kwani amekuwa akijitoa kwa mambo mengi juu ya wenye mahitaji.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments