SLIM AANDIKA HISTORIA TEMEKE


Na Shushu Joel, Temeke


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam Ndugu Khamis Slim ameandika historia katika jumuiya hiyo kwa kuendesha jumuiya hiyo kidijitali. 



Akizungumza katika Baraza la kanuni la Jumuiya hiyo Slim alisema kuwa jumuiya yake itagawa kompyuta mpakato kwa makatibu wote wa kata ili ziweze kurahisisha utendaji wa kazi zao za Jumuiya na chama kwa ujumla.


Aidha aliongeza kuwa kabla ya kugawa vifaa hivyo kutakuwa na semina elekezi juu ya matumizi ya kompyuta hizo ili iweze kuwa vyepesi kwao kwa matumizi yao ya utendaji.


Pia Mwenyekiti huyo alisema kuwa ni vyema sasa kila kiongozi akajifunza matumizi ya mifumo ya kisasa kwani tunakoelekea digital inaenda kuwa na nafasi kubwa katika jamii.


Naye Abel Mkingwa mjumbe wa mkutano huo amemsifu Mwenyekiti kwa jinsi ambavo amekuwa shupavu katika kuongoza jumùiya hiyo


MWIßĤO

Post a Comment

0 Comments