WAZIRI LUKUVI AMWAKILISHA RAIS DKT SAMIA IBADA YA KUMUOMBEA HAYATI DKT MAGUFULI CHATO

Na Mwandishi wetu 

Leo Machi 17, 2025 ni kumbukizi ya miaka 4 toka kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya 5 Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Wilayani Chato mkoani Geita kumefanyika misa takatifu ya kumuombea ambapo familia ya Hayati Magufuli ikiongozwa na mjane wake Mama Janeth Magufuli na viongozi mbalimbali wa kitaifa, mkoa na Chama wameshiriki. 



Misa hiyo ya ibada ya kumuombea Hayati Magufuli imefanyika katika Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara Parokia ya Mt. Yohana Maria Muzeyi Mlimani huku Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ibada hiyo. 


Viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Naibu Katibu Mkuu CCM Taifa Ndugu John Mongela, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Innocent Bashungwa, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Rehema Sombi na wengine wa Chama na Serikali wamehudhuria misa hiyo.

Post a Comment

0 Comments