Na Shushu Joel, Bagamoyo
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Abubakar Mlawa amewataka wana chama wa Chama hicho kuacha tabia ya makundi ndani ya chama mara moja kwani yatakizorotesha.
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akitoa neno la shukurani mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm Bagamoyo akichukua nafasi ya Sharifu .
" Tabia ya kuwa na makundi ndani ya chama ni mbaya sana kwani itakigawa chama vipande vipande hivyo kama Mwenhekiti wenu nawaombeni kuacha mara moja tabia hiyo" Alisema Mlawa.
Aidha Mwenhekiti huyo amewakumbusha wanachama hao kurudisha heshima ya ccm ndani ya wilaya ya Bagamoyo ambapo miaka ya nyuma Bagamoyo kinara wa kila jambo hapa Nchini.
Pia Mlawa amewakumbusha wana ccm kuendelea kuyasema maendeleo yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Samia Suluhu Hassan .
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya Ndugu Mkwayu Makoto amempongeza Mwenhekiti kwa ushindi na kueleza kuwa wana ccm na wananchi wa Bagamoyo wanamatumaini makubwa na uongozi wake.
MWISHO
0 Comments