DKT MANDAI AHAMASISHA KUZIISHI R4 ZA RAIS DKT SAMIA KWA WAPINZANI KIGAMBONI


Na Shushu Joel, Kigamboni 

π‘¨π’”π’Šπ’”π’Šπ’•π’Šπ’›π’‚ π’Œπ’–π’…π’–π’Žπ’Šπ’”π’‰π’‚ π‘¨π’Žπ’‚π’π’Š π’Œπ’˜π’‚ π‘½π’Šπ’•π’†π’π’…π’


Mjumbe wa Baraza kuu Wazazi Taifa (viti 3- Bara) Dkt. Ally Mandai, ameendelea kutoa somo la kuziishi kwa vitendo Falsafa ya R4 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Wana CCM na Wapinzani Nchini.



Dkt. Mandai amesema kuwa, " _kazi ya kuleta maendeleo siyo ya mtu mmoja, tunahitajiana wote kwa pamoja pakiwepo na Amani, Utulivu na Mshikamano_ ".


Dkt. Mandai amesisitiza kuwa " _Tukiendelea kushikamana kama wana CCM na Wasio wana CCM (Upinzani) Taifa letu litaendelea kupaa kimaendeleo"._


" _Uongozi wetu iwe sababu ya watu kuungana na siyo watu kutengana_ ".


" _Uongozi wetu uhubiri R4 za Mhe. Rais Samia ili kuwaponya wanaohubiri makundi ndani yetu CCM lakini pia na Wapinzani._ "


Aidha, Dkt. Mandai amewataka Wana CCM kuendelea kuwaelimisha na kuwapokea Wapinzani kwa maslahi mapana ya Taifa.


#KaziNaUtuTunasongaMbele

Post a Comment

0 Comments