Na Shushu Joel, Kisarawe.
MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa anayetokana na Umoja wa Wanawake Tanzania Bi Nadra Ghulam ametoa maagizo kwa viongozi wa Mamlaka ya maji wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani kuhakikisha wanawapatia huduma wananchi kwa wakati.
Maagizo hayo ameyatoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Chole Wilaya ya Kisarawe katika mwendelezo wa ziara ya umoja wa Wanawake Tanzania ambapo Mnec alipangiwa kata hiyo.
Aidha alisema kuwa ni vyema wananchi wakapatiwa huduma ya maji kwa wakati ili kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi wa eneo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amezipatia pesa za kutosha mamlaka za maji kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanapatiwa huduma hizo kwa wakati huku lengo la kumtua mama ndoa linatimia.
Katika kikao hicho Mnec Nadra Ghulam alimpigia simu Meneja wa mamlaka hiyo ya maji kutaka kujua lini tatizo hilo linakwenda kutatuliwa ndipo meneja alimwakikishia kuwa ndani ya mwezi huu changamoto hiyo inakwenda kukamilika na ukosekanaji wa maji unakwenda kuwa historia katika kata hiyo.
Naye Khadija Juma amempongeza Mnec Nadra Ghulam kwa jinsi ambavyo amekuwa akitatua kero za wananchi kwa njia ya simu huku zingine akizimaliza hapo hapo.
Aidha alisema kuwa viongozi wa chama ambao wanafanana na Mnec Nadra Ghulam ni wachache hivyo huyu ni lulu kubwa lazima tuitunze na kuilinda.
MWISHO
0 Comments