DC KAWAWA ATAKA MTUMISHI BANDARI YA BAGAMOYO AONDOLEWE.

Na shushu joel

MKUU wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Zainabu Kawawa ameitaka mamlaka ya Bandari nchini(TPA) kumuondoa mtumishi ambaye amekuwa ni kero kwa wafanyabiashara katika wilaya hiyo.


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa akifafanua jambo mbele ya wafanyabiashaara wa bandarini(PICHA NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza na wafanyabiashara wa bandari ya Bagamoyo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa mfanyakazi huyo wa TPA amekuwa ni kero kubwa kwa wafanyakazi hao kutokana na manyanyaso makubwa anayowafanyia wafanyabiashara wa eneo hilo kwani anafikia hatua ya kuwapiga wenzake huku kwenye uongozi jambo hilo hakuna.

Aliongeza kuwa awali serikali ya wilaya ilikuwa ikipambana na wimbi la vijana ambao walikimbia kwenye bandari hiyo na kukimbilia mtaani ambako walikuwa wakifanya mambo ya ovyo ingawa serikali iliwachukulia hatua kali za  kinidhamu na kuacha tabia hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa(SHUSHU JOEL)
"Vijana wanaobeba mizigo wamekuwa wakisumbuliwa na mtumishi huyo na hivyo kupelekea vijana hao kuhama hama hivyo mtu huyu hafai kuwepo kwenye wilaya ya Bagamoyo kwani ananyanyasa vijana wangu kwa kuwafanya wakimbilie msituni "Alisema Kawawa.

Pia Kawawa aliongeza kuwa amewaomba wafanyakazi hao kuendelea na shughuli zao za kila siku katika eneo hilo kwani mtumishi huyo ni lazima aondoke kutokana na kuwanyanyasa wafanyabiashara kwenye eneo hilo pia kuikosesha wilaya mapato.

Aidha Kawawa amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na TAKUKURU kwenda kwenye bandari hiyo na kutaka kuwakamata wafanyabiashara hao kwa kosa la kukwepa kodi kitu ambacho sio sahihi kwao.


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa akisisitiza jambo
Alisema kuwa mambo yote haya yanayofanywa na TAKUKURU pamoja na huyo mtumishi kumekuwa na sintofahau na hivyo kuwataka kutoendelea na tabia hiyo

Kwa upande wake Afisa forodha wa bandari hiyo ya Bagamoyo alisema kuwa  wamefanikiwa kukamata madumu ya mafuta ambayo yalikuwa yakikwepeshwa kulipa kodi.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments