WAZIRI ULEGA AMWAGUKIA JPM.


Na shushu joel

NAIBU Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega ameomba kujengewa kwa barabara ya kisasa ili magari ya mwendo kasi yaweze kufika katika wilaya hiyo ili kurahisisha shughuli za wananchi wa halmashauri hiyo.

Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi Abdalaah Ulega akifafanua jambo.
Ombi hilo amelitoa katika shughuli za uzinduzi wa mradi wa maji katika wilaya ya kisarawe mkoani Pwani ambapo Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizindua mradi huo.

Akizungumza mbele ya umati wa wananchi wa mkoa wa Pwani na viongozi mbalimbali Ulega ameomba barabara ya mwendo kasi na kituo cha mabasi ili kuwasaidia wananchi wa kusini wanaopata changamoto lukuki kwa kukosa sehemu maalumu ya kituo cha kupandia na kushukia wakiwa wanatoka katika mikoa ya Mtwara,Lindi na Ruvuma.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza jambo katika moja ya mikutano ya Bunge
"Mkuranga wakati unaingia madarakani ulikuwa na viwanda 20 tu lakini leo mkuranga inaviwanda 97 pia ilikuwa inakusanya Bilioni 3.5 ya Tra lakini sasa makusanyo yetu yamepanda na kukusanya zaidi ya Bilion 15"Alisema Ulega.

Aidha aliongeza alimwakikishia kuwa wilaya ya Mkuranga imetenga eneo la hekari zaidi ya 100 hivyo wanaomba kupelekewa mahitaji hayo walioyaomba kwa ajili ya upanuzi wa wilaya ya Mkuranga.


Naye Said Majiwa(83) amempongeza Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli kwa utendaji wa kazi uliotukuka na hasa kwa kuwajali wanyonge.

Aidha alisema kuwa wana Mkuranga wanaamini maombi yaliyotolewa na Mbunge wao juu ya maombi ya Stand,na kufika kwa barabara ya mwendo kasi yatafanikiwa kutokana na usikuvu wa Rais Dkt Magufuli.

Naye Bibi Tochi (78) ambaye ni mkazi wa kijiji cha kitonga amemsifu Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa jinsi anavyopambana na nchi hii kwani amekuwa mkombozi wa wanawake kwa kujenga vituo vya Afya Nchi nzima


Aliongeza kuwa kama mambo haya yanayofanywa na Dkt Magufuli ingekuwa enzi zao wangekuwa na nafasi kubwa ya kuwa na watoto wengi wenye afya njema kutokana na uwepo wa huduma karibu.

Aidha amempongeza mbunge wa Mkuranga ambaye pia Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Abdallah Ulega kwani ameipendezesha Mkuranga kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa huduma za kijamii za uhakika ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo wabunge wengi walikuwa wakijinufaisha matumbo yap tu bila kuwajali wananchi wao.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Ulega akifafanua jambo
"Wananchi wenzangu viongozi kama kina Ulega ni wachache na wanatokea mara moja moja hivyo tuwashikilie watatuvusha na kuacha alama kubwa katika halmashauri yetu ya Mkuranga"Alisema Bibi Tochi.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments