MBUNGE wa jimbo la Chalinze,wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Mh Ridhiwani Kikwete amefanikiwa kutatua changamoto kubwa iliyokuwa imedumu kwa kipindi kirefu katika kata ya Mbwewe ya kutokupatikana kwa maji safi na salama.
![]() |
Mbunge wa jimbo la chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akimtwisha moja wa kina mama waliojitokeza katika hafla ya kukabidhi mradi huo wa kisima kirefu(PICHA NA SHUSHU JOEL) |
"Katika kipindi cha miaka mitano tumefanikiwa kutatua kero kubwa ya Maji ambayo awali ilikuwa ni aibu kwa uongozi wetu uliokuwepo kwani wananchi wetu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze walikuwa wakinywa maji na wanyama"Alisema Kikwete.
![]() |
Mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete akipeana mkono na mwenyekiti wa CCM kata hiyo mara baada ya kukabidhiwa kwa kisima hicho(SHUSHU JOEL) |
Aidha Mh.Kikwete aliwataka wananchi wa Chalinze kuhakikisha wanavilinda visima na mabwawa hayo ili viendelee kutumika huku wakisubili kuanza kwa mradi mkubwa wa maji wa Chalinze Wami ambao upo kwenye hatua za mwisho.
Pia katika hali nyengine Mh. Kikwete ameipongeza na Kuishukuru kampuni ya uchimbaji wa visima ya Bin Shomari Co.Ltd kwa msaada mkubwa wa ushirikiano wa uchimbaji wa visima na mabwawa katika maeneo mbalimbali Ndani ya Halmashauri ya Chalinze.
![]() |
Mh Mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wananchi mara baada ya kukabidhi mradi huo wa maji. |
Naye Mh. Diwani Ndugu Malota Kwaga wa kata ya kiwangwa ambaye pia ni mwenyekiti wa huduma za kijamii amempongeza na kusifu juhudi za Mbunge kwa kuhakikisha wananchi wa Chalinze wanapata huduma bora hasa katika maeneo ya Huduma Maji, Afya, Elimu, Mikopo na jinsi alivyowez kujitoa kusaidia kwenye kuangahika pale inapohitajika kuongeza nguvu serikali au nguvu ya wananchi.
Aliongeza kuwa katika kata yake ya kiwangwa palikuwa na uhaba mkubwa wa maji lakini kipindi hiki cha miaka mitano changamoto hizo zimebaki kuwa ni historia kwa sasa . Juhudi hizi zinazofanyika ni muhimu sana kuziunga mkono ili tuendelee kufaidi matunda ya uongozi mzuri wa Mbunge wetu.
Naye Bi.Aisha Iddy mkazi wa Kwaruhombo amempongeza mbunge wa jimbo hilo kwa kuwafanya kinamama wa eneo hilo kurudisha furaha majumbani kwani uhaba wa maji ulikuwa mkubwa sana huku viongozi waliokuwepo madarakani wakituangalia tu.
![]() |
Mkurugenzi wa kampuni ya Bin Shomari Ltd wakipeana mikono mara baada ya kukabidhiana kisima hicho |
Aidha amesema kuwa uongozi wa kikwete ni wa mfano na tutaendelea nae mpaka aache mwenyewe kutokana na yale tunayoyataka yafanyike yanafanikiwa.
Huku kwa upande wa Viongozi wa Chama , Mwenyekiti wa Ccm wa kata ya Mbwewe ndugu Idadi Ally alimshukuru sana Mbunge kwa kuwasaidia kutatua kero hiyo na kwa kufanya hivyo amekipa sababu Chama Cha Mapinduzi kusema bila ya ukakasi inapokuwa kwenye kunadi mambo yaliyotekelezwa na Chama.
MWISHO
0 Comments