MCHOPA AWATAKA WATUMISHI KUPUNGUZA UZITO.


Na shushu joel

WATUMISHI wa halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wametakiwa kupima uzito wa miili yao ili kujua Afya zao.

Rai hiyo imetolewa na mratibu wa huduma ya mama na mtoto Bertha Mchopa alipokuwa katika zoezi la uhamasishaji wa kupima uzito kwa watumishi wa halmashauri ya Chalinze.

Mratibu wa mama na mtoto Bi,Bertha Mchopa akimpima uzito Afisa habari wa halmashauri ya chalinze John Mlyambate(PICHA NA SHUSHU JOEL)
Mchopa alisema kuwa watumishi walio wengi tumekuwa na changamoto ya uzito mkubwa hivyo kupelekea kukumbwa na matatizo ya magonjwa yasiyo ya lazima.

"Uzito unapokuwa tofauti na kimo cha mwili wako inakuwa ni shida kubwa kwani uwiano wa mwili na uzito unatofautiana hivyo unaweza kuwa unasikia maumivu ya mwili mara kwa mara"Alisema  Mchopa.

Aidha aliongeza kuwa mara baada ya kujua uzito wako unatakiwa kuzingatia vyakula visivyo na mafuta ili kuepuka kunenepa kwa mwili pasipo kuwa na sababu za msingi.

Kwa upande wake Afisa habari wa halmashauri hiyo John Mlyambate ambaye alikuwa wa kwanza kupima uzito wake amewapongeza wataalamu hao kwa kutambua umuhimu wa kutoa elimu kwa watumishi.


 Aidha amewataka watumishi wenzake kujitoa ili kuhakikisha wanapima uzito wa miili yao na kujua namna jinsi ya kuweka mwili katika hali inayotakiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Lishe  ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze Bi Zainab Makwinya.amempongeza mratibu wa zoezi hilo la utoaji wa elimu kwa watumishi kujua uzito wao.


 Aidha amemtaka mratibu huyo pindi atakapofika kwa wananchi awaeleze ukweli kuwa zoezi hili lilianzia kwa watumishi kwani wao pia wanachangamoto hiyo ya kutokuthamini lishe sitahiki .

MWISHO

Post a Comment

0 Comments