Na Bahati Sonda, Simiyu.
Mjumbe wa Bodi ya Mradi wa Umeme vijijini hapa nchini (REA) Mhandisi Styden Rwebangila amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya utendaji wa mkandarasi anayetekeleza mradi huo wa awamu 3 katika Mkoa wa Simiyu unaotarajiwa kuisha mapema mwezi agosti mwaka huu ambayo ni miradi ya kimkakati Kanda ya Ziwa.
Mhandisi Rwebangila ameyabainisha hayo mapema jana katika ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya 3 na kusema kuwa ameridhishwa na kasi ya utendaji kazi kwani vijiji 106 kati ya 153 vimeunganishiwa hivyo kufikia mwezi agosti vilivyobaki vitakuwa tayari
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Umeme hapa nchini wa Mkoa (Tanesco) wakimsikiliza mjumbe wa bodi ya Mradi wa Umeme vijijini REA Mhandisi Styden Rwebangila (hayupo pichani) kwenye kikao kifupi kilichofanyika kwenye ofisi za Tanesco Mkoa wa Simiyu zilizopo mjini Bariadi.
" Nimeridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa mkandarasi anayetekeleza mradi REA 3 mkoani Simiyu kwani tayari amekwisha unganisha vijiji 106 ambapo vimebaki vijiji 47 tu hivyo ninaamini muda ambao umebaki unatosha kumaliza" Alisema mhandisi Rwebangila
Naye Mkandarasi anayetekeleza mradi wa REA awamu ya 3 mkoani hapa Cathbert Shirima kutoka Kampuni ya Whitecity Guardong alizitaja changamoto kubwa alizokabiliana nazo wakati wa kutekeleza mradi wake ni miundombinu mibaya ambayo ilipelekea kushindwa kutekelezwa kwa miradi kwenye baadhi ya vijiji pamoja na ubovu wa barabara hususan katika kipindi cha masika hali iliyopelekea miradi kusimama na kushindwa kutekelezeka kwa wakati.
![]() |
| Vifaa vya kutekekezea mradi wa Umeme vijijini hapa nchini (REA) vikipakiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa kwenye maeneo mbalimbali ya mradi huo |
Aidha mkandarasi Rwebangila akizungumzia changamoto ya ubovu wa miundombinu alimtaka mkandarasi kuhakikisha anajiridhisha mapema kabla ya kuzipeleka anazipima na kujiridhisha mapema hususan nguo kabla ya kuzipeleka kwenye maeneo ya utekelezaji miradi kwani tayari bodi ilishaifanyia kazi changamoto hiyo.
Awali Meneja wa Shirika la Umeme Mkoani Simiyu(Tanesco) mhandisi
Khadija Abdallahmed alisema kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza kutokana na changamoto kubwa kuwa kukosekana kwa mawasiliano baina ya mkandarasi na ofisi za Tanesco pamoja na mkandarasi na viongozi wa maeneo husika ambao wangeweza kutatua baadhi ya changamoto zinazojitokeza wakati wa kutekeleza mradi.
" Changamoto kubwa iliyojitokeza ni kukosekana kwa mawasiliano baina ya mkandarasi na ofisi za Tanesco pamoja na viongozi wa maeneo husika hivyo tumeichukua na tutaifanyia kazi" Alisema mhandisi Abdallahmed
Kwa upande wao wanufaika wa mradi huo akiwemo Kubugu Bunzari mkazi wa kijiji cha Ibulyu mjini Bariadi aliishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa rais Dkt John Magufuli kwa kutatua tatizo lililikuwa likiwasumbua kwani kabla ya kupata umeme wa REA walikuwa wanatumia mafuta ya taa ambayo walijikuta wakitumia gharama kubwa kuliko umeme.
![]() |
| Vifaa vya umeme vya kutekekezea mradi wa Umeme vijijini (REA) awamu ya 3 mkoani Simiyu vikiwa vimewekwa kwenye stoo yake iliyopo mtaa wa Kidinda mjini Bariadi |
" Kabla ya kupata umeme huu wa REA tulikuwa tunatumia mafuta ya taa ambapo kwa lita 1 tulikuwa tunanunua kwa shilingi 3000 na kwamba lita hiyo moja ilikuwa inatumika kwa wiki 1 tu kwa hiyo kwa mwezi mzima tulikuwa tunatumia kiasi cha shilingi 12000 ambapo kwa sasa tunatumia umeme wa 5000 tu na hatuumalizi kwa mwezi" Alisema Bunzari
Naye Catherine Makongoro mkazi wa Mtaa wa Nyangaka uliopo mjini Bariadi alibainisha kuwa awali kabla ya kupata umeme huo walikuwa wakitumia solar ambazo nazo zilikuwa zikiharibika na kujikuta wakinunua mara kwa mara ambapo changamoto hiyo imetatuliwa na mradi wa umeme vijijini.
" Nipende kuishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa rais Dkt Magufuli kwa mradi huu ambao umetusaidia kwani awali tulikuwa tunatumia solar ambazo nazo zilikuwa zikiharibika mara kwa mara na kwamba tulikuwa tunatumia gharama kubwa sana " Alisema Makongoro
Mwisho.




0 Comments