UTEKELEZAJI WA ILANI CHALINZE WAVUTA UTITILI WA WANACHAMA KUJIUNGA CCM

Na shushu joel

MIAKA mitano ya Mafanikio makubwa katika utekelezaji wa Ilani ndani ya Halmashauri ya Chalinze katika kipindi cha Miaka Mitano (2015-2020) chini ya Uongozi wa Mbunge Mh. Ridhiwani Jakaya Kikwete kumezaa Neema ambapo wananchama wengi wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mbunge wa jimbo la chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akisalimiana na mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na CCM(PICHA NA SHUSHU JOEL)
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanachama hao wapya wa Chama Cha Mapinduzi wamepongeza utekelezaji wa ilani katika halmashauri ya Chalinze na hiyo kuwa ndiyo sababu kubwa ya wao kuvutiwa kujiunga na Chama hicho. Wanachama hao ambao wengi wao ni watumishi 26 wa shule moja iliyopo Chalinze wameeleza kuwa utekelezaji wa Ilani ndiyo sababu kubwa iliyowasukuma  kujiunga na CCM.

Bw, Paschal ambaye ni Mwalimu alieleza kuwa wao wameridhika kutokana na uelekeo mzuri wa utatuzi wa kero za wananchi. 

Ameeleza kuvutiwa na miradi inayotekelezwa kimataifa na kihalmashauri kama utatuzi wa kero ya Maji, upatikanaji wa huduma za afya karibu nao, usalama wa raia na mali zao, ukuaji wa sekta ya elimu, mahusiano mema na serikali ya kijiji na chama wanapokuwa na changamoto zao kuwa ni moja kati ya Vitu vilivyowavutia. Akieleza hayo kwa niaba ya Wanachama wenzake alimpongeza Mwenyekiti wa Chama wa Chama Wilaya kwa kusimamia utekelezaji na huku akimpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa Ubunifu wake alishirikiana na madiwani wake.

Mbunge wa jimbo la chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akizungumzia utekelezaji wa Ilani wa jimbo hilo mbele ya viongozi wa CCM  pamoja na wanachama wapya waliojuinga na chama hicho(PICHA NA SHUSHU JOEL)
 Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao wapya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ndg. Abdul-Zahoro Sharif alisema kuwa Ccm imefanya  vizuri kwa kipindi kirefu lakini mafanikio haya ndani ya miaka mitano ni zawadi kwa wananchi na ndiyo maana watanzania wenye uelewa wamekuwa wakimiminika kujiunga na chama hicho kwa mapenzi yao wenyewe.

"Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Mbunge wa jimbo letu la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete wamekuwa msaada mkubwa katika Chama kwani utekelezaji wa ahadi za Chama kwa wananchi. Furaha yangu ni kuwa Ilani tumeikamilisha kwa asilimia zaidi ya 95%" Alisema Mwenyekiti Zahoro.

Aidha  Mwenyekiti huyo wa CCM wilaya ya Bagamoyo alitumia nafasi hiyo kuwaonya wale wanaotamani kuona Shughuli za Chama zinasimama kwa sababu ya maslahi yao ya kisiasa. Mwenyekiti Zahoro, alitumia nafasi hiyo kuwasihi sana maafisa wa Vyombo vinavyofuatilia mienendo ya Uchaguzi ndani ya Chama kufanya kazi yao kwa uadilifu Mkubwa na huku wakiache chama kitimize wajibu wake. Mwenyekiti Zahoro alisema," ... niwataadharishe sana watumishi wa vyombo watambue kuwa Shughuli za Chama hazijazimama hivyo wafanye kazi wakijua kuwa chama kinafanya kazi zake na hiki si Chama cha Uchaguzi."

Mmoja wa wanachama wapya aliyetambulika kwa jina moja la Bi. Rehema alisema kuwa sababu ya yeye kujiunga na Chama ni mabadiliko makubwa yanayoonekana katika  jimbo la Chalinze ukianza kwenye huduma za afya,Nishati, elimu, miundombinu, vifaa tiba. Jimbo la Chalinze limebadilika sana tofauti na miaka ya nyuma kwani sasa kila huduma zinapatikana kwa urahisi na wepesi na hizi zote ni juhudi za mbunge wa jimbo".

Mbunge wa chalinze Mh Ridhiwani Kikwete mwenye Tsheti ya njano akiongoza furaha za wanachama wapya waliojiunga na CCM (PICHA NA SHUSHU JOEL)



Naye Mbunge wa jimbo hilo Mh. Ridhiwani Kikwete aliwaasa wanachama hao wapya kutqmbua kuwa wao ni jeshi la chama kwenda kukisemea katika Umma. Katika tukio jengine Mh. Mbunge aliwakabidhi wanachama hao taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Miaka mitano (2015-2020) ili wafahamu mazuri yaliyofanywa na Serikali katika awamu hii ya tano ya uongozi wa nchi.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments