MKUU wa Mkoa wa Pwani Eng Evarist Ndikilo amemsifu mbunge wa jimbo la Chalinze Ndg Ridhiwani Kikwete kwa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi(CCm) kwa asilimia 98% kwenye miradi mbalimbali kwa ajili ya wananchi.
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akipokea kitabu cha utekelezaji wa Ilani kutoka kwa mbunge wa jimbo la chalinze Mh Ridhiwani Kikwete(NA SHUSHU JOEL) |
Mkuu wa Mkoa alieleza kuwa mafanikio yaliyopatikana kwa ujenzi wa vituo vya Afya, Zahanati na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze, Ujenzi wa Miundo mbinu ya umeme takribani kila kijiji,miundombinu ya barabara kuhakikisha kuwa zinapitika muda wote, kupatikana kwa maji na mabadiliko ya uendeshaki wa shughuli za upatikanaji wa Maji kiurahisi na uimarishaji wa Elimu, upatikanaji wa Mamlaka kamili ya Wilaya ya Chalinze ni kwa sehemu kubwa Mchango wa Mheshimiwa Mbunge ambao unatokana na mahusiano makubwa ambayo yamejengwa na Mheshimiwa Mbunge akishirikiana na Serikali katika kuhakikisha Wananchi wake wanapata faida ya kuchagua Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Aliongeza kuwa Kikwete amekuwa kiunganishi kikibwa baina ya serikali na wananchi kwani amekuwa akiwasemea sana Wananchi wake bungeni na kubisha hodi ofisi mbalimbali za Serikali hasa kwangu na za mawaziri kwa lengo la kujua jimbo lake linafaidikaje na Fursa zilizopo.
"Katika mkoa wangu wa Pwani jimbo la Chalinze ndio limekuwa la kwanza katika utekelezaji wa ilani ya CCM kutokana na kile ambacho tulikuwa tukikihitaji kifanyike kimefanyika na wananchi wanaendelea kutumia miradi hiyo"Alisema Eng Ndikilo.
![]() |
Mlezi wa mkoa wa Pwani CCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa wanawake Gaudencia Kabaka naye akipokea kitabu cha utekelezaji kutoka kwa Mbunge wa jimbo la chalinze Mh Ridhiwani Kikwete(PICHA NA SHUSHU JOEL) |
Kwa upande wa Mlezi wa Mkoa huo , Mama Gaudensia Kabata Ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakinamama wa Chama Cha Mapinduzi alimpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kazi Nzuri ambayo inayoa nafasi kwa wagombea wa chama kujinadi bila wasi wowote. Lakini kwa upekee kabisa alimshukuru sana kwa msaada mkubwa aliputoa kuhakikisha jamii ya kifugaji inarudi kwenye amani kwa kurudisha Kijiji, kuwahangaikia eneo la malisho na kuwezesha kuanza kwa majadiliano ya kupungua gharama ya kukodisha vitalu.
![]() |
Mama Gaudencia Kabaka akiwa pamoja na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo kulia na mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete. |
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya mstaafu wa wilaya ya Kibaya Assumter Mshama amempongeza mbunge huyo kwa uchapakazi wake uliotukuka kwa wananchi wake na kumtaka kuendelea na moyo huyo kwani wananchi ndio wanajua walipokuwa siku za nyuma na walipo sasa kwani kila yaliyofanyika katika jimbo hilo analoliongoza yanaonekana wazi.
![]() |
Mama Kabaka akisikiliza maelezo ya mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete mara baada ya kumkabidhi kitabu cha utekelezaji wa ilani |
Mheshimiwa Mbunge alikumbusba kuwa kama isingalikuwa mafiga matati ya ushirikiano isingeliwezekana haya. Aliongeza kuwa utekelezaji uliofanyika chalinze ni shirikishi baina ya nguzo tatu ambazo ni wananchi, wawakilishi na serikali.
Aidha Kikwete amemsifu Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwa nguzo yake katika ufanikishaji wa maendeleo kwenye jimbo la chalinze hasa katika kukabiliana na changamoto za wananchi katika wilaya yao na pia kusisistiza wananchi wajiandae kwa ajili ya yanayokuja ambayo ni makubwa sana.
"Serikali ya awamu ya Tano chini ya Dkt Magufuli imekuwa bega kwa bega na Chalinze ndio maana imetupatia fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali inayolenga kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero zilizokuwa zikiwasumbua awali"Alisema Kikwete.
MWISHO
0 Comments