MADIWANI wapya sita wa Viti Maalumu kwenye Tarafa 7 zilizopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wamechomoza katika kura za maoni zilizofanyika Julai 27 wilayani hapa.
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) wilaya ya Bagamoyo Hanipha Checheta akitoa maelekezo kwa wagombea (NA SHUSHU JOEL) |
Chini ya Usimamizi Juma Gama Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoani hapa akisaidiwa na Katibu wa (CCM) Gertrude Sinyinza, UWT iliwakilishwa na Hanipha Checheta Katibu na Lukhia Masenga Mwenyekiti wa Jumuia hiyo ukishuhudiwa na Kamati ya Siasa wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti Abdul Sharifu.
Baadhi ya wajumbe wa UWT wakifuatilia sera za wagombea kwa makini(NA SHUSHU JOEL) |
Tarafa ya Miono Sijali Mpwimbwi akiibuka tena katika nafasi hiyo kwa kura 449 dhidi ya Esther Helman 84, Tunu Mpwimbwi 421 amerejea Tarafa ya Kwaruhombo, huku Mwanakesi Madega 381 aking'ara Chalinze akiunga na sura mpya Tatu Mpogo 278, wakimuongoza Upendo Moreto 197.
Mmoja wa wagombea akijinadi mbele ya wajumbe.NA SHUSHU JOEL) |
Baada ya zoezi hilo Gama aliwaambia wajumbe hao kuwa kwenye zoezi hilo hakuna mshindi, kwani majina yote yatasubiri vikao vya ngazi za juu vitavyokuja na maamuzi ya nani ataipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba.
Mgombea wa udiwani viti maalum akitoa sera zake kwa wajumbe kabla ya kupigiwa kura(PICHA NA SHUSHU JOEL) |
MWISHO
0 Comments