FUGENI NYUKI WAWAONDOE KWENYE UMASIKINI:SAGIN

Na Shushu Joel Simiyu.

WANANCHI  wameshauriwa kufuga nyuki ili waweze kujiongezea kipato na
kuwainua kiuchumi na hivyo kuondokana na umasikini kwa kuwa ufugaji
huo ni moja ya shughuli za maendeleo.

Ushauri huo umetolewa na aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini alipokuwa akizunguka kwenye baadhi ya Mabanda ya Maonyesho ya Nane Nane kwenye viwanja vya Nyakabidndi qilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu ambapo sherehe hizo zinafanyika kitaifa Mkoani hapa.

Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini akiangalia jinsi ya kutengeneza Mizinga ya nyuki ya kisasa na ya bei Nafuu.(NA SHUSHU JOEL)
Alisema kuwa maeneo ambayo wananchi wanafanya shughuli za ufugaji wa nyuki  hiyo ni fursa nzuri wanayoipata ni vizuri wakaitumia kwa uzalishaji kuliko kutegemea kila kitu kufanyiwa na serikali ili waweze kuondokana na umasikini hasa kwa wananchi waishiyo maeneo ya vijijini.

“Ukifuga nyuki niwahakikishie wananchi kuiwa mtaagana na umasikinikwani kuna faida nyingi utazipata kwani unaweza kupata asali pamoja na Nta ambazo  zina bei kubwa kulingana na mahitaji yake ”alisema.m Sagini.

Alisema kuwa licha ya faida hizo ambazo mfugaji anaweza kuzipata pia ufugaji huo hutumika katika utunzaji wa mazingira kwani maeneo ambayo imewekwa mizinga kwa ajili ya kuwafuga nyuki hao hakuna shughuli za kibinadamu zinazoweza kufanyika kama vile ukataji ovyo wa miti kwani nyuki ni walinzi wazuri sana.

Jumanne Sagini akifurahu jambo na waandishi wa habari hawapo pichani(SHUSHU JOEL)Add caption
 “Ufugaji wa nyuki huhifadhi mazingira kwani kwa kutundika mizinga ya nyuki  kwenye misitu wananchi  wanashindwa  kuvamia misitu hiyo na wale wavamizi wakorofi wanaovamia misitu hiyo hukabiliana na nyuki kwa kuumwa hivyo hawa ni walinzi wazuri sana wa misitu yetu”alisema.

Alisema kuwa halmashauri za wilaya takribani zote nchini zinawataalamu wa ufugaji nyuki hivyo naamini wanaendelea na utoaji elimu kwa jamii imekuwa ikitoa hivyo nawaomba wajitahidi kuwaelezea wananchi wao kwa lengo la kunufaika na nyuki hao.

Naye Grace Kalunde ambaye ni mfugaji wa nyuki kutoka kijiji cha
Ipililo wilayani humo alisema kuwa katika kijiji chao wameunda kikundi chao chao kinachojishughulisha na ufugaji wa nyuki na kwa sasa wanayo mizinga185 iliyotundikwa  na wanatarajia kuvuna kiasi cha kilo 2500 za asali na Nta kilo 278.

‘Matarajio ya uvunaji wa mazao ya nyuki tunategemea kuvuna kiasi cha kilo 2500 na Nta kilo 278 na katika soko la sasa bei ya kilo moja ya asali ni Sh 10,000 hadi Sh 12,000 na Nta ni Sh 15,000 hadi Sh 25,000/= kwa kilo,”alisema.


Alisema kuwa Mradi wa ufugaji wa nyuki katika kijiji hicho
unawahusisha wanakikundi wapatao 27 kati yao wamawake 11 na wanaume 16 na zaidi ya kiasi cha fedha Sh Milioni 30 zilitolewa kama mkopo na halmashauri ya wilaya ya Maswa ili waweze kufanya shughuli hizo za ufugaji wa nyuki.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments