WANANCHI WATAKIWA KUWA WALINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME:MWENYEKI BODI YA REA

Na shushu joel, Simiyu

MWENYEKITI wa Bodi ya Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo amewataka wananchi wa Mkoa wa Simiyu kuwa walinzi na wasimamizi wa miundombinu ya umeme ili iweze kuwanufaisha katika maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi waliokuwa wamejitokeza kwenye banda la maonyesho la TANESCO huku wakihoji juu ya umeme wa REA.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini,Wakili Julius Kalolo akifafanua jambo kuhusu faida za umeme mbele ya waandishi wa Habari hawapo pichana(PICHA NA SHUSHU JOEL)
 Wakili Kalolo aliongeza kuwa  kumekuwa na tabia kwa baadhi ya sehemu kwa kuhisi kuwa mara baada ya serikali kutengeneza miundombinu ya umeme basi na mwagalizi wake anapaswa kuwa ni serikali wakati wao ndio wahudumiwa wakuu wa mradi huo.

"Naipongeza serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa usikivu wake wa haraka kwani mahitaji yetu yamekuwa yakitekelezwa kwa haraka na hivyo nasi kutimiza wajibu wetu wetu kwa wananchi "Alisema Wakili Kalolo.

Meneja wa TANESCO mkoa wa Simiyu Khadija Abdallahm akisisitiza jambo kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda hilo hawapo pichaniAdd caption
Aidha aliongeza kuwa mpaka sasa REA imesambaza umeme vijijini kwa asilimia zaidi ya 80% na hivyo kupelekea vijiji vichache tu ambavyo havikufikiwa kwa awamu hii ingawa katika kipindi kinachokuja cha REA tumejiwekea malengo kuwa ifikapo mwezi wa sita mwakani tutakuwa tumefika kila kitongoji.

Aliongeza kuwa wananchi mnatakiwa kutambua kuwa umeme una faida kubwa katika kujiongezea kipata kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo hivyo niwaombe mchangamkie fursa hii.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini Wakili Kalolo akifafanua jambo kwa wananhi juu ya ulinzi wa miundombinu ya umeme.
Naye Meneja wa Tanesco Mkoawa Simiyu Khadija Abdalalahm amemueleza Mwenyekiti huyo wa Bodi kuwa shirika la umeme nchini lipo makini katika kutekeleza utendaji wake na hasa kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa Umeme.

Aidha aliwataka pia wananchi kuwa walinzi wa kila mmoja ili kila mradi uweze kuendelevu.

Afisa wa shirika la umeme Tanesco akiwaelekeza baadhi wanafunzi waliojitokeza kwenye shirika hilo ili kujua jinsi umeme unavyowasaidia wananchi.

Naye Minza Masanyiwa mkazi wa Bariadi vijijini ambaye alikuja kwenye banda la Tanesco alisema kuwa ameweza kupata elimu juu ya matumizi ya umeme pia anashukuru kwa kujua kuwa hata nyumba ya nyasi inawekewa umeme,hivyo amemuomba meneja wa mkoa kuzunguka na MMETA kwani jamii sasa inahitaji umeme.

MWISHO

 

Post a Comment

0 Comments