Na shushu joel, Simiyu
MKUU wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amewataka wananchi wa mkoa huo kuchangamkia fursa zinazojitokeza kwenye maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Nyakabidi ili ziweze kuwanufaisha katika shughuli zao za uzalishaji majumbani kwao.
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akitembea kwenye baadhi ya mabanda ya taasisi mbalimbali zilizojitokeza kwenye maonyesho hayo ya Nane Nane.
"Mwaka huu kumekuwa na vitu vingi vya kujifunza na vyenye tija kubwa kwa watu wa Simiyu hivyo kila mmoja wetu anatakiwa kununua kile kinachostahili kwa ajili ya uendeshaji wa kazi zake "Alisema Mtaka.Baadhi ya kifaa kinachotumika kwa ajili ya kilimo na shughuli mbalimbali mashambani(Trecka)NA SHUSHU JOEL
Aliongeza kuwa kwa wakulima kuna kila aina ya vitendea kazi kwa ajili ya shughuli za kilimo chenye tija kubwa kwa ajili ya kilimo cha Biashara na chakula.
Aidha Mtaka aliongeza kuwa kwenye maonyesho hayo kuna dawa nyingi za kuua wadudu waaribifu mashambani hivyo hii ni neema kwetu wana Simiyu na tunapaswa kuitumia kwa maendeleo ya mkoa wetu kwa kuongeza kipato kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji na uimara wa vitendea kazi.
Kwa upande wake Mmoja wa wakulima bora kutoka wilaya ya Maswa Mathias Masangu alisema kuwa maonyesha ya kipindi hiki ni neema kubwa kwetu wakulima wa zao la pamba kwani kuna kila aina ya elimu inatolewa kutoka kwenye taasisi mbalimbali za kilimo na hata wale wauzaji wa vifaa.Moja ya Treka za kisasa zilizopo kwenye maonyesho ya nane nane kwenye viwanja vya Nyakabindi(NA SHUSHU JOEL)
Alisema kuwa Kilimo cha Pamba kinahitaji uangalizi wa hali ya juu hivyo kila yule mwenye nia ya kuhitaji kunufaika na kilimo cha zao hilo anapaswa kuzingatia kanuni za kilimo bora za pamba.
"Nimekuwa mkulima bora kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo hivyo wakulima wenzangu zingatieni kanuni tu za kilimo mtafanikiwa "Alisema Masonga.Moja ya kifaa cha kupandia mbegu za mbunga kwa njia ya kisasa kinachopatikana kwenye viwanja vya Nane Nane .
Aidha aliongeza kuwa Nane Nane imekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Simiyu.
MWISHO
0 Comments