Na shushu joel
KADA wa chama cha mapinduzi(CCM) na aliyekuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Simiyu Simon Songe amefanikiwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Busega.
Fomu hizo amekabidhiwa majira ya mchana na msimamizi msaidizi wa uchaguzi ngazi ya wilaya Bw,Gidion Bunto.Bw,Simon Songe akifurahi jambo na msimamizi wa uchaguzi hayupo pichani.(PICHA NA SHUSHU JOEL)
Awali msimamizi huyo wa uchaguzi alimkabidhi mgombea huyo fomu mbili ambazo moja ni ya maadili ambayo ujazwa mbele ya msimamizi huyo huku nyingine ni kwa ajili ya nafasi aliyepewa na chama chake cha ccm ya Ubunge.
Songe alishukuru Mungu kwa chama na viongozi wakuu wa wa chama hicho kwa kurejesha jina lake ili aweze kupeperusha bendera huku akisema kuwa jambo la kamati kuu kumuamini ni heshima kubwa sana kwake huku akisema kuwa wananchi wa Busega watarajie kupata maendeleo makubwa waliyokuwa wakiyahitaji na kuyalilia miaka yote.Msimamizi wa uchaguzi kulia Gidion Bunto akimkabidhi fomu ya ugombea ubunge Simon Songe kushota(PICHA NA SHUSHU JOEL)
Aliongeza kuwa kipindi hiki cha uongozi wake wakazi wa Busega watarajie kupata mambo makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu,Miundombinu,Afya na Maji.
Songe alisema kuwa kikubwa ni kutafuta wadau kwa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha miradi ambayo ilikuwa ni sugu katika jimbo hili inakamilika na kuwa msaada kwa wakazi wa maeneo husika.Simon Songe akimsikiliza kwa makini msimamizi wa uchaguzi huku Mwenezi wa ccm Samwel Ngofilo akishuhudia tukio hilo.
"Nimekuwa nikiona changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikishindwa kutatuliwa na viongozi watangulizi lakini niwahakikishie wananchi wenzangu wa Busega hivyo tukifanya umoja wa maendeleo tutakuwa na Busega ya mfano kwenye taifa hili"Alisema
Aliongeza kuwa atakuwa msumbufu sana kwa viongozi wa juu kwa lengo la kuwafanikishia wananchi wake kile wanachokihitaji I kifanyike na kiwe na tija kwa jamii.Samwel Ngofilo ambaye ni katibu mwenezi wa ccm wilaya ya Busega akihakiki fomu alizopewa mgombea wa ubunge wa ccm jimbo la Busega Simon Songe na msimamizi wa uchaguzi.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Busega Samwel Ngofilo alisema kuwa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu kikubwa ni ushirikiano kwa wana ccm ili kuhakikisha chama hicho kinaibuka na ushindi wa kishindo kwenye nafasi za Rais,Ubunge na Diwani.Simon Songe akitabasamu mara baada ya kukutana na baadhi ya wajumbe wa chama hicho.
MWISHO
1 Comments
Kila la kheri ndugu yangu Songe Mungu akufanyie wepesi katika safari yako ya uongozi wa busega na taifa kwa jumla.
ReplyDelete