UDSM WAJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUFUKUZA WANYAMA NA NDEGE MASHAMBANI.

Na Shushu Joel,Simiyu

Chuo kikuu Cha Dar es salaaam, kimekuja na teknolojia mpya ambazo zimelenga kuwanufaisha wakulima pamoja na kuwapunguzia adha wanazokutana nazo katika shughuli zao za mashambani .

Teknolojia hizo zimeonyeshwa katika maonyesho ya nane nane yanayoendelea kitaifa katika mkoa wa Simiyu, ambapo watalamu hao wameonyesha namna ambavyo wamekuja na mbinu mpya ili kuwasaidia wakulima na wavuvi katika kutatua changamoto zao zinazowakabili,

Dr Athumani Mahinda (PHD) kutoka Chuo Kikuu cha Udsm akionyesha kifaa hicho chenye uwezo wa kufukuza wanya na ndege waaribifu mashambani.(NA SHUSHU JOEL)

Akionyesha kifaa maalum cha kufukuza ndege mashambani Dr Athumani Mahinda(PHD)alisema kuwa kifaa hiki ni mahususi katika kufukuza ndege na wanyama wakali mashambani kwani kinatumia upepo tu hivyo upepo unapovuma upiga kelel za aina yake na hivyo upelekea wanyama na ndege wote kukimbia .

Aliongeza kuwa kitaalamu unashauriwa kutumia vifaa 4 kwa hekta moja ili kila kona unaweka kifaa hiki.

Akionyesha mfumo mpya wa manunuzi na uuzaji wa samaki kwa njia ya mtandao Ester Mhamila mwanafunzi wa viumbe maji na uvuvi alisema, kuwa kwa kutambua adha wanazozipata wavuvi Katia kuuza bidhaa zao sokoni wameamua kuwarauisishia huduma.

Dr Athumani Mahinda akifafanua jamba mble ya waandishi wa habari juu ya matumizi ya kifaa hicho chenye uwezo mkubwa wa kupambana na wanyama pamoja na ndege.(SHUSHU JOEL)
 "Tumeanzisha program ya fishgenge ambayo wavuvi wataitumia kuuza samaki na wanunuzi kununua samaki kwa Bei inayohitajika eleweka kupitia Application inayopatika katika simu za mkonono," alisema.

 

Aliongeza kuwa mbali na kufanya manunuzi vile vile mnunuzi atapata nafasi ya kuona aina ya samaki anao wahitaji wanavirutubisho vya aina gani ili kumuongezea uelewa mzuri wa virutubishi vilivyopo katika samaki.

 

Watalamu hao pia wanateknolojia ya kuzuia wadudu waharibifu katika maharage ambapo kea kutumia majani ya mimea Ambayo haitumii kemikali yeyote na mazao yanakuwa salama kwa miezi mitatu Hadi minne.

Kifaa chenyewe kikionekana kwa karibu kikiwa kimetulia huku kikisubili upepo ili kianze kuvuma
 "Tunatumia majani ya mimea ya mwarobaini na utupa katika kuhifadhi maharage, majani hayo inatakiwa isagwe vizuri Kisha ikaushwe baadaye mkulima atachanganya na maharage,"alifafanua Joseph Kalonga Mhadhili Msaidizi was ndaki ya sayansi ya kilimo na uvuvi.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments