WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UPIMAJI WA MASIKINI

 Na Anita Balingilaki ,Bariadi

Zaidi ya wananchi 100 wamefikiwa na huduma ya uchunguzi wa masikio inayotolewa na wataalam kutoka chuo kikuu  cha askofu mkuu Mihayo cha mkiani Tabora ambacho ni tawi la SAUTI Tanzania kwenya viwanja vya maonesho ya nane nane yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu.



Hayo yamesemwa na mhadhiri wa chuo hicho sister Dkt Sophia Mbihije na kuongeza kuwa  chuo chao kinatoa elimu shahada mbalimbali ikiwemo , elimu ya uchunguzi wa masikio , elimu mahitaji maalum ,shahada ya Sanaa katika elimu na shahada ya utawala katika biashara na wako kwenye maonesho hayo ili waweze kuwashirikisha wananchi umuhimu wa shahada hizo ambazo ni za muhimu sana katika kuielimisha jamii hasa hasa shahada ya elimu mahitaji maalum

Lukonge John akitoa huduma ya upimaji wa sikio kwa mmoja wa wananchi aliyefika kupata huduma hiyo(NA ANITA)

Amesema chuo hicho kinafundisha uchunguzi wa masikio ili kujua nini chanzo cha tatizo na namna ya kulitatua na muhitimu akitoka hapo ataweza kuajiriwa au  kujiajiri na kusaidia wenye mahitaji hayo.

 Aidha ameongeza kuwa wanawatayarisha walimu ambao wataweza kufundisha shule za sekondari ili kukidhi mahitaji ya watoto wenye mahitaji maalum hususan viziwi na wasioona na ili mwalimu aweze kumuhudumia mwanafunzi kitaaluma wanahitaji ajue lugha ya alama na huyu mwanafunzi akiishajua lugha hii itamsaidia na yeye badae kuwa mkarimani na si katika kitengo cha elimu tu lakini pia katika ofisi mbalimbali za umma na binafsi.

wanazotoa ni pamoja na kutayarisha walimu wenye uwezo wa kufundisha wenye mahitaji maalum mfano viziwi na wasioona ili badae wawe wataalamu wa kukarumani .

Sister Dkt Sophia Mbihije akitoa elimu kwa wananchi wakiwemo wanafunzi kwenye maonyesho ya Nane Nane
 

Aidha ameongeza kuwa elimu hiyo itawasaidia kujiajiri na kuajiriwa kwenye sekta /taasisi  mbalimbali zikiwemo za umma na binafsi .
Katika hatua nyingine ameongeza kuwa ni matumaini yao kupitia maonesho hayo wananchi wataitikia kufika kwenye banda lao kupata elimu ya namna ya kujiunga na chuo hicho sambamba na kupata huduma ya kupima masikio bure.

Lukonge John kutoka chuo hicho  amesema tangu wafike kwenye maonesho hayo wameweza kuwahudumia watu mbalimbali huku asilimia kubwa ikitoka kanda ya ziwa na kuongeza kuwa  amewakaribisha wazazi na walezi kuchangamkia fursa hiyo ya kupima masikio bure pamoja na kujiunga na chuo chao ambapo amesema vigezo vya kujiunga sio vigezo tofauti mtu akiwa na principle mbili anauwezo wa kujiunga kidato cha sita au aliyemaliza stashahada  mwenye GPA  ya 3 na kuendelea

Baadhi ya vifaa vinavyotumiwa na Sister Dkt Mbihije wakati wa kutoa huduma kwa jamii.

Na baadhi ya wananchi waliotembelea bsnda hilo hususan wenye matatizo ya masikio wamesema huduma zinazotolewa ni za uhakika na hazina gharama yoyote.

MWISHO

Post a Comment

1 Comments

  1. Hongera Sana team Amucta kwa kuindeleza taaluma hii tuko pamoja ktk kukitangaza chuo chetu

    ReplyDelete