WAJASILIAMALI 1200 WAFIKIWA

Na Anita Balingilaki ,

 Wajasiliamali 1200 wamefikiwa tangu kuanzishwa kwa kliniki ya biashara ambayo ina zaidi ya miaka miwili tangu kuanzishwa

Afisa Biashara wa TANTRADE Gilbert Waigama akizungumza jambo na baadhi ya wateja waliotembelea Banda hilo(ANITA)
 Hayo yamesemwa na afisa biashara kutoka TANTRADE Gilbert Waigama wakati akizungumza na waandishi wa habari kusema kuwa tangu kuanzishwa kwa kliniki hiyo mwitikio umekuwa mkubwa kwa wafanyabiashara wadogo na wakati ambapo wamerasimisha biashara zao huku akiongeza kuwa biashara iliyo rasmi inakopesheka .

Mbali na hayo ameongeza kuwa jumla ya wataalam 16 kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi zipo kwenye maonesho ya nanenane yanayofanyika kitaifa viwanja vya nyakabindi vilivyopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu hivyo ni vema wananchi hususan wafanyabiashara kutumia fursa ya maonesho hayo.
Watoaji wa Huduma kutoka srkta mbalimbali za serikali wakiwa tayari kwa kugfanya kazi
Waigama alisema wanahusika na kutatua kero mbalimbali hususan za wale ambao biashara zao zinashindwa kukua sambamba na kuwawezesha kupata mazingira wezeshi.

Katika hatua nyingine amesema changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na baadhi ya wateja kutoa taarifa nusu nusu au ambazo hazina uhakika.

mwisho..

Post a Comment

0 Comments