Na Shushu Joel,Simiyu.
WANANCHI mbalimbali wa Mkoa wa Simiyu wanaozidi kujionea maajabu mengi yanayojitokeza kwenye maonyesho ya Nane Nane mkoa humo wamekiri ya kuwa kila jambo linalofanyika mkoa humo chanzo chake ni mkuu wa mkoa wao.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye viwanja vya Nane Nane Nyakabindi(SHUSHU JOEL) |
Nkali Suluja (54) mkazi wa Ngasamo wilaya ya Busega Mkoani humo alisema kuwa maonyesho ya nanenane yamekuwa msaada mkubwa kwa wanasimiyu kutokana na yale yanayotendeka kwenye Mkoa wetu wa Simiyu kwa juhudi za Mkuu wa Mkoa
![]() |
Nkali Suluja mwenye kofia akipata maelekezo ya jinsi ya kufuga samaki na kuweza kuondokana na changamoto za maisha kutoka kwa Afisa Mifugo wilaya ya Maswa. |
Aidha aliongeza kuwa miaka ya nyuma mkoa wa simiyu ulikuwa na viongozi wa juu lakini uwepo wa Mtaka umechangia kukua na kuimarika kwa mkoa wetu ikiwemo viwanda,kukua kwa elimu kuimarika kwa ulinzi na usalama ndani ya mkoa wetu.
![]() |
Moja wa Ng'ombe wa kisasa waliopo kwenye maonyesho ya Nane Nane Simiyu. |
Kwa upande wake Tabitha Masanja aliyefika kwenye maonyesho ya Nane Nane kwenye viwanja vya Nyakabindi kwa mara ya kwanza anasema kuwa kwa kweli nimejionea mambo mengi mazuri ambayo nilikuwa sijawai kuona kwenye maisha yangu kutokana na kuwa maonyesha yalikuwa yakifanyika mbali na makazi yetu.
Aliongeza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anton Mtaka amekuwa nguzo kubwa kwa wakazi wa Simiyu kutokana na upambanaji wake wa kazi kwa kuwafungulia fursa nyingi wakazi wa Mkoa uo kwa ujumla
![]() |
Bi Tabitha Masanja mwenye mtoto kushoto akiangalia jinsi ya kufuga samaki kwa njia ya kisasa |
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anton Mtaka alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema kuwa yeye ni mtendaji wa serikali hivyo ni wajibu wake kuhakikisha wananchi wa mkoa wake wanapata fursa za kutosha kutoka serikalini na kwa wadau mbalimbali .
Aidha aliongeza kuwa yeye peke yake asingeweza kufanya jambo lolote lile bali ni ushirikiano mkubwa anaoupata kutoka kwa wasaidizi wake pamoja na wananchi ambao wamekuwa msaada mkubwa kwa kuhakikisha Simiyu inasonga mbele kwenye maendeleo.
![]() |
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kujionea jinsi gani unaweza kufuga samaki kwa njia ya kisasa na kuweza kujipatia kipato |
“Kauli mbiu ya Nane Nane kwa mwaka huu iko wazi na inasema kuwa kwa Maendeleo ya Kilimo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020”
MWISHO
0 Comments