WANANCHI WAKILI BADO WANAIMANI KUBWA NA KIKWETE

Na Shushu joel

WANANCHI wa halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wamesema kuwa bado wanaimani kubwa na mwakilishi katika uletaji wa maendeleo katika jimbo hilo.

Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wananchi walisema kuwa kipindi cha miaka 5 iliyopita mwakilishi wao  amefanikiwa kutekelezaji ahadi kubwa za maendeleo.

Baadhi ya wananchi wa jimbo la chalinze wakifurahia jambo na mwakilishi wao (Mbunge) Mh Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia CCM.(PICHA NA SHUSHU JOEL)
Juma Ally(45) ni mkazi wa Miono alisema kuwa kuelekea kipindi hiki cha miaka 5 ijayo tunaimani kubwa na Ridhiwani Kikwete kutokana na kuwa amekuwa mstali wa mbele kwenye ufanikishaji wa maendeleo katika jimbo.

Baadhi ya wana chama wa chama cha mapinduzi ccm wakifurahia jambo na mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete.(NA SHUSHU JOEL)
 

Aidha aliongeza kuwa Kikwete amekuwa mkombozi wa wananchi wa chalinze kwa kugusa nyanja mbalimbali za kimaendeleo .

Mwajuma Hemed alisema kuwa kwa upande wetu Wanawake wa chalinze tumefanikiwa kuwa na sehemu nyingi za kupata huduma kutokana na kuwepo kwa miradi ya Afya kuanzia ngazi za kijiji huku kikubwa zaidi ni kuwepo kwa  vifaa vya kutosha.

Mbunge wa jimbo la chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akikabidhi fomu kwa mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya chalinze Ramadhani Posi(NA SHUSHU JOEL)
 

Aidha alisema kuwa mitano ijayo itakuwa ni neema kubwa kwa wananchi wa Chalinze kutokana na mitano ya nyuma kuwa ya neema hivyo ijayo itazidishi neema kwa wakazi wa chalinze.

Naye Ridhiwani Kikwete amesema kuwa anaimani kubwa na wananchi wake hivyo hakuna kitakacho halibika kwenye ufanikishaji wa maendeleo.

MWISHO

Post a Comment

1 Comments