KIKWETE ANOGESHA MBIO ZA KUSAKA KURA ZA DKT MAGUFULI.

Na shushu joel,Chalinze.

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze anayesubili kuapishwa Mh. Ridhiwani Jakaya Kikwete ameendelea na kampeni za kumuombea kura Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Dkt. John Pombe Magufuli kwa wananchi wa Jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa kata ya Vigwaza alipokuwa akiwaomba kumpigia kura za kutosha Dkt Magufuli ili aendelee kuwa Rais kwa kipindi kingine(PICHA NA SHUSHU JOEL)
 
Akizungumza na wananchi wa kata ya Vigwaza Mh. Kikwete alisema kuwa kuna sababu nyingi za kumpatia kura za kishindo Dkt Magufuli ili aendelee kuwa Rais wetu kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo. "Tumejipanga vizuri ili kuhakikisha Rais wetu Dkt. Magufuli anapata kura za kishindo kikubwa chenye heshima kwenye Jimbo letu la chalinze"Alisema Kikwete.

Aidha alisema kuwa miradi mingi  iliyotekelezwa hapa Chalinze inatosha kutoa ishara kuwa kiongozi mkuu wa nchi yetu ametufanyia mengi mazuri na hivyo wananchi wenzangu nawaomba tumpatie kura nyingi za heshima Dkt Magufuli ili aendelee kutuletea maendeleo katika Jimbo letu.

Mbunge wa Chalinze anayesubili kuapisha Ridhiwani Kikwete pamoja na baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM  wakiwa wameshika picha ya Mgombea Urais Dkt Magufuli wakionyesha ishara ya ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi ujao.(NA SHUSHU JOEL)
 
Kwa upande wake Katibu  wa kata ya vigwaza kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Ndg. Ameir  alisema kuwa kura za Rais Dkt Magufuli zipo za kutosha kwani wananchi wa kata yetu wanasubilia siku tu ili wakamwagie Kura Dkt Magufuli.

Tunamshukuru sana Mheshimiwa Raisi wetu amekuwa wa msaada mkubwa sana sio tu kwa Watanzania lakini kwa wananchi wa Chalinze kwa jumla.

Baadhi ya vijana na wapenzi wa chama cha mapinduzi (CCM)wakiwa wakiwa wameshika picha za mabango ya Dkt Magufuli(NA SHUSHU JOEL)
   


Naye Haji Jumbe mkazi wa Vigwaza alisema kuwa kwa niaba ya wananchi wamejipanga ili kuhakikisha kura za Dkt Magufuli zinakuwa za kutosha ili aendelee kuwapatia maendeleo.

Alisema kuwa kutokana na kupewa kwa maendeleo ya kutosha katika Jimbo la Chalinze nasi zawadi yetu kubwa ni kjmpigia kura za kutosha Dkt Magufuli ili aendelee kuwatumikia watanzania wanyonge.

"Mbunge wetu Ndg. Kikwete tunakuomba kutokuwa na wasiwasi juu yetu kwani kazi zako ulizozifanya za kutuletea Maji, Umeme, Miundombinu na huduma za Afya zimekuwa imara tofauti na miaka ya nyuma hivyo tutatoa  Kura za kutosha"Alisema Jumbe.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na moja wa wazee maarufu katika kata ya Vigwaza mara baada ya mkutano(.NA SHUSHU JOEL)

 
Aidha alisema kuwa mbali na kutekelezeka kwa miradi kumekuwa na uwezesho mkubwa kwa vijana,mama na watu wenye ulemavu katika Jimbo letu na kupelekea makundi hayo kunufaika na mikopo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments