Na Anita Balingilaki, Simiyu
Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama mkoani Simiyu unatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 51% mwaka 2019 hadi 57.4 % ifikapo 0ctoba 2020 kupitia mradi wa Programu kwa matokeo ya (PF4R ) hali itakayosaidia wananchi kupata huduma hiyo kwa uhakika na urahisi.
Mbali na ongezeko hilo pia kutakuwepo na ongezeko la ajira kwa wananchi ambao watajipatia kazi kupitia mradi wa usambazazji wa mabomba katika miradi 23 itakayotekelezwa.
Hayo yamesemwa leo na meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) mhandisi Mariam Majala wakati wa makabidhiano ya mabomba yatakayotumika kutekeleza miradi ya mji mkoani humo yaliyofanyika katika ofisi za RUWASA mjini Bariadi.
Mhandisi Majala alisema mpaka sasa wamepokea 70 % ya mabomba ya maji yenye thamani ya milioni 823 ambayo yatatumika kutekeleza miradi 23 kwa mkoa mzima huku wakisubiria wakati wowote kuwasili kwa 30 % ya mabomba yaliyobaki.
" hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa sasa sio mbaya na nawahakikishia wananchi ongezeko kubwa la huduma hiyo" alisema Mhandisi Majala.
eneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini ( RUWASA) mhandisi Mariam Majala akionesha mabomba
Awali
akikagua mabomba haya katibu tawala mkoa wa Simiyu Mariam Mmbaga aliwataka
wananchi kushiriki kwenye mradi huo kwa kutunza miundombinu ya maji ili lengo
la ongezeko hilo walilokusudia liweze kufikiwa
huku akiipongeza bodi ya manunuzi kwa kazi nzuri iliyofanyika.
" niwatake wananchi wa mkoa huu ( Simiyu) kuitunza miundombinu ya maji inayotekelezwa na serikali ili iweze kudumu na kuwanufaisha wote kama ilivyokusudiwa"alisema Mmbaga
Baadhi ya mabomba yatakayotumika kwenye utekelezaji.
Kwa upande wake mjumbe wa bodi manunuzi Ekwabi Mujungu ameomba kazi ifanyike kama ilivyopagwa ili thamani ya fedha ionekane .
MWISHO
0 Comments