Na Shushu Joel,Busega.
MGOMBEA wa nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM) katika Jimbo la Busega Mkoani Simiyu Simon Songe amewaahidi neema wananchi wa kata ya Mwamanyili pindi watakapompigia kura na kuwa mshindi katika nafasi ya ubunge kwenye Jimbo hilo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu Simon Songe akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa CCM(NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza na umati wa wananchi waliojitokeza katika mwendelezo wa kampeni za kuomba kura za Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli,Nafasi ya Ubunge na madiwani Songe alisema kuwa wakazi wa Mwamanyili watapata huduma zote za jamii katika kipindi hiki kutokana na serikali ya CCM ilivyo kusudia kuwahudumia wananchi wake.
Aliongeza kuwa kumekuwa na changamoto za ukosekanaji wa maji ya kutosha kwa jamii,miundombinu,umeme na Afya hivyo nawaomba wananchi wa mwamanyili kuichagua ccm ili iweze kuwafanikishia pale palipobakia.
Umati wa wananchi wa Mwamanyili waliojitokeza kumsikiliza mbunge wa Jimbo hilo Simon Songe(NA SHUSHU JOEL)
“Mafiga matatu ndio mpango mzima yaani Rais wa CCM,Mbunge wa CCM,na madiwani wa CCM kwa maendeleo ya Busega “Alisema Songe.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa chama cha mapinduzi(CCM) wilaya hiyo Samweli Ngofilo alisema kuwa kura za kishindo zinakuja Busega hivyo cha msingi kila mwananchi ajitokeze kwenda kupiga kura siku hiyo.
Aidha amewapongeza wananchi wa mwamanyili kwa kujitokeza kwenye mkutano na kusikiliza sera za CCM .
Simon Songe mgombea wa ubunge Busega kulia na Katibu Mwenezi wa CCM kushoto wakifurahia jambo mara baada ya mkutano wa kuomba kura Mwamanyili.(SHUSHU JOEL)
Naye Malimi Suluja amekipongeza chama cha mapinduzi(CCM) kwa kunadi sera safi na zenye kueleweka kwa wananchi wa kata hiyo.
Aliongeza kuwa kwa yale yaliyosemwa na wagombea ni kweli kabisa CCM inamakusudi makubwa kwa wananchi wa Mwamanyili juu ya maendeleo yao.
MWISHO
0 Comments