KIKWETE:DKT MAGUFULI KIMBILIO LETU WANA CHALINZE.

 Na shushu joel, Chalinze.

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete awewakumbusha wananchi wake wa Jimbo hilo kuhakikisha wanampigia kura za kutosha Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM)  Dkt John Pombe Magufuli kwani ndio kimbilio letu wanachalinze.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Bwilingu Mh.Kikwete alisema kuwa miaka mitano iliyopita Rais Dkt Magufuli ametutendea makubwa wana Chalinze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Afya,Miundombinu,Maji na Umeme na hivi ndivyo vilikuwa vilio vyetu vikubwa katika Jimbo letu.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa kata ya Bwilingu ambapo Kikwete ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi hao kuchagua mafiga matatu yaani Rais Mbunge na Diwani wote wa CCM ingawa yeye amepita tayari.(NA SHUSHU JJOEL)

Aliongeza kuwa awali jimbo letu lilikuwa na changamoto nyingi za upatikanaji wa huduma za kijamii,lakini katika utawala wa Rais Dkt Magufuli Jimbo la Chalinze limekuwa na neema kubwa kwa wananchi wa Chalinze katika nyanja mbalimbali za maisha.

 

Aidha aliwaasa wananchi wenzake kukumbuka  maendeleo yaliyoletwa na CCM na hayo yawe  chachu ya kutusukuma tumpe kura nyingi sana.  "hivyo niwaombe kwa mimi kama Mbunge wenu nawaombeni muchague mafiga matatu ili maendeleo yaweze kufika kwa haraka"Alisema Kikwete. Mheshimiwa Mbunge aliongeza kuwa Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele na amesimamia misingi na ni mpenda maendeleo yetu,anayewajali wanyonge.

Kwa upande wake Mgombea Udiwani wa kata ya Bwilingu Nassar Karama kupitia chama cha mapinduzi(CCM) amemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo Mh Ridhiwani Kikwete kwa jinsi amekuwa msaada mkubwa kwa kusimamia maendeeo ya jimbo lake na kuhakikisha zile changamoto za maisha ya wanachalinze zinatatuliwa katika muda.

Aidha Ndugu Karama alisema kuwa anaamini kura zitakuwa nyingi kutoka kwa wananchi kwani wamesha onja mafanikio ya kuwa na viongozi wa CCM.

Naye Bi' Zena Selemani(79)amewahakikishia viongozi hao kuwa hakuna  mwananchi yeyote yule wa Chalinze wa kumnyima kura Rais Dkt Magufuli na Diwani Nasser kutokana na kuwa chama cha mapinduzi kina sera nzuri na zenye tija kwa jamii na kubwa zaidi ni kazi nauri iliyokwisha fanyika.

Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akimkabidhi mgombea udiwani kata ya Bwilingu Nassar Karama Ilani ya ccm ya mwaka 2020 mpaka 2025.(SHUSHU JOEL)

Aidha alisema kuwa kwa Jimbo letu la Chalinze hakuna mwananchi ambaye ajaona maendeleo yaliyofanywa na Mbunge wetu kwani maji,huduma za Afya,Umeme na Miundombinu imeimalika mara dufu ya miaka ya nyuma.

 

"Enzi hizo maji ilikuwa ni historia lakini kipindi hiki hakuna aja ya kuwa na mindoo mingi ndani huku maji yakiwa yanatoka mara zote kwenye mabomba "Alisema  Bi'Zena.

 

MWISHO

Post a Comment

0 Comments