SONGE: DR. MAGUFULI KIMBILIO LETU BUSEGA.

 Na Shushu Joel,Busega.

MGOMBEA Ubunge katika Jimbo la Busega Mkoani Simiyu kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Mh.Simon Songe amewakumbusha wananchi wake wa Jimbo hilo kuhakikisha wanampigia kura za kutosho Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dr.John Pombe Magufuli kwani ndiye kimbilio letu wananchi wa Busega.

Akizungumza na wananchi wa kata ya kiloleli Mh Songe alisema kuwa miaka mitano iliyopita Rais Dr.Magufuli ametutendea makubwa wananchi wa Busega kwani neema kubwa imemiminika kwa wakazi wa Busega kwa kunufaika kupata miradi mbalimbali.

Mgombea ubunge wa jimbo la Busega Simon Songe akizungumza na wananchi wa kata ya kiloleli(NA SHUSHU JOEL)
  

Aidha Songe aliwaaasa wananchi wenzake kukumbuka maendeleo yaliyoletwa na CCM na hayo yawe chachu ya kuweza kuendelea kutusukuma kumpa kura nyingi na za kishindo.

:Hivyo niwaombe mimi kama mbunge wenu mtarajiwa muweze kuchagua mafiga matatu ili maendeleo yaweze kufika kwa haraka”Alisema Songe

Aliongeza kuwa Dr. Magufuli amekuwa ni kiongozi wa pekee mwenye kupenda wanyonge na mwenye kusimamaia maendeleo ya jamii pasipo ubaguzi wa aina yeyote ile.

Kwa Upande wake Mgombea udiwani wa kata hiyo Ndugu Vumi Magoti kupitia chama cha mapinduzi (CCM) amemshukuru Mgombea ubunge wa Jimbo hilo Mh Songe kwa jinsi amekuwa msaada mkubwa  katika kusimamia maendeleo ya Jimbo la Busega.

Simon Songe akimuombea kura Dr.Magufuli kwa wananchi wa kata ya kiloleli(NA SHUSHU JOEL)
 

Aidha Mgulila alisema kuwa anaamini kuwa kura zitakuwa ni nyindi kutoka kwa wananchi wa kiloleli za kumchagua Dr.Magufuli kwa yale mazuri aliyoyafanya.

Naye Bi,Susana Malimi(65) amewahakikishia viongozi hao kuwa hakuna mwananchi yeyote Yule wa Busega wa kumnyima kura Dr.Magufuli,Mbunge Songe na Diwani Mgulila hii ni kutokana na kuwa chama cha mapinduzi kina sera nzuri na zenye tija kwa jamii.

Aidha aliongeza kuwa katika jimbo letu la Busega Hakuna mwanachi ambaye ajaona maendeleo yaliyofanywa na ccm kwani Afya,miundombinu ,umeme na maji vinaonekana.

MWISHO

 

Post a Comment

0 Comments