Na Shushu Joel,Busega
MGOMBEA Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Busega Mkoani Simiyu Simon Songe amewahakikishia wananchi wa kata ya Mkula kuwa pindi watakampo mpatia nafasi ya kuwa mwakilishi wao kwenye Bunge la Tanzania atahakikisha changamoto kubwa zinazowakabili wakazi hao zinabaki kuwa ni historia.
Akizungumza na wananchi hao Songe alisema kuwa huduma ya Afya imekuwa ni changamoto kubwa kwa wakazi wa kata hii kutokana na usimamizi mbovu wa maendeleo uliokuwepo awali lakini niwahakikishie wananchi wa mkula kuwa pindi mtakaponipatia nafasi ya kuwa mwakilishi wenu jambo la kwanza ni kuimalika kwa huduma hiyo ya Afya na ile ya maji.

Simon Songe akizungumza na wananchi wa kata ya Mkula(NA SHUSHU JOEL)
Aliongeza kuwa msiwachague watu wasio kuwa na ilani kwani watawarudisha utumwani hivyo kila mmoja wetu awe mstali wa mbele kuhakikisha kila mwana mkula anampigia kura Dr.John Pombe Magufuli ili aendelee kuliongoza taifa hili kwa kipindi kingine cha miaka mitano pia kumchagua diwani wa CCM na Mbunge wa chama hicho.
Aidha Songe alisema kuwa ni chama kimoja tu chenye uwezo wa kuwavusha wanachi katika maendeleo ya dhati.
Kwa upande wake Bi,Shabo Bukombe(62) amempongeza Songe kwa ahadi zake kwa wananchi wa kata hiyo kwani ametugusa wanawake moja kwa moja kutokana na kuwa wao ndio wahenga wakubwa katika huduma za Afya na huduna za maji.
Aliongeza
kuwa Songe atafanikiwa kwa kuwa anaonekana ni kiongozi mwenye hofu ya Mungu
hivyo wananchi wenzangu jitokezeni siku hiyo kuipigia kura CCM ili ituletee
maendeleo.

Baadhi ya wananchi wa kata ya mkula wakimsikiliza mgombea ubunge Simon Songe(NA SHUSHU JOEL)
Nzumbi Magembe alisema kuwa mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa kituo cha Afya katika kata ya Mkula kutasaidia kinamama na watoto ambao awali walikuwa wakipatiwa huduma hizo kwenye Hospital binafsi na hivyo gharama zimekuwa ni kubwa huku wananchi wengi wao ni wanyonge.
Aliongeza kuwa pia maji yakianza kutoka kwenye eneo hilo Songe atakuwa ni mbunge wa kudumu kutokana na kuwa atakuwa amefanikiwa kuutafuna mfupa uliowashinda viongozi wengi.
MWISHO

0 Comments