DR. MAGUFULI KUPATA KURA KEDEKEDE CHALINZE.

Na Shushu Joel,Chalinze.


WANANCHI wa kata ya Miono,Jimbo la Chalinze limemtaka Mbunge wa Jimbo hilo Mh Ridhiwani Kikwete kutembea kifua mbele na kujiandaa kwenda Bungeni kwa furaha kubwa kutokana na kura nyingi na za kutosha zitakazopigwa kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na wagombea wake ili kiendelee kushika madaraka na kutuletea maendeleo wananchi wake siku ya tarehe 28 Oktoba 2020.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa kata ya Miono ambapo walimwakikishia mbunge kura zao zote kwa Dr.Magufuli(NA SHUSHU JOEL)
 
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wananchi hao walisema , wanatambua mambo mengi ya thamani kubwa waliyofanyiwa na chama hicho hivyo ni lazima kipindi hiki wakipatie kura nyingi ili waweze kuendelea kuleta maendeleo kwa faida yao.

Ndg. Omary Hussein (78) mkazi wa kijiji cha Machala ambaye alifurahi sana kumuona Mbunge wake ambaye alimtambulisha kama Mchapa kqzi Imara asiyeyumba, mwenye msimamo alisema kuwa tangu ujana wake hajawai kukosea kupiga kura kwa wapinzani kutokana na kuwa chama cha mapinduzi kimekuwa ni tegemezi na lulu kwa jamii. Ndugu Omary Aliongeza kuwa Mgombea Urais kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli ni kiongozi wa mfano mzuri wa kuigwa  sio tu katika Afrika bali hata katika mataifa mbalimbali kwa utendaji wake wa kazi. 

Aliongeza pia vitendo vyake vya kuthamini wanyonge waliokuwa wakionewa na watu wenye pesa huku wengine wakiachwa bila mwelekea wa aina yeyote kinampa nafasi ya kipekee kwa wananchi sisi.Itakapofika tarehe hiyo tutaenda kupiga kura kwa Dr. Magufuli ili aweze kuendelea kuwa kiongozi wa Tanzania mwenye kupenda na kuthamani maendeleo kwa jamii husika. “Kura yangu mimi,mke wangu mimi,watoto wangu na majirani zangu wote kura zao zote watahakikisha wanampigia kura Dkt Magufuli” Alisema.



Naye Bi.Khadija Juma (57) amempongeza Mh Ridhiwani Kikwete kwa kupita bila kupingwa,hii yote ni wapinzani kuona jinsi gani kazi zimefanyika katika jimbo la Chalinze.
Aliongeza kuwa juhudi anazozifanya mbunge kwa sasa za kusaka kura za Dr. Magufuli ni nzuri lakini sie kama wananchi tukuhakikishie tu kuwa uchaguzi ulishakwisha kwetu bado kuapishwa tu kwa viongozi wetu.

Mh.Ridhiwani Kikwete Mbunge anayesubili kuapishwa akiomba kura za Rais Dr.Magufuli kwenye mkutano kata ya Miono.
 

Aidha amewataka kina mama kukumbuka mazuri yanayofanywa na CCM kwenye kijiji chao na kata yao ususani ni kwenye Elimu, Afya, mikopo kwa wakina mama na vijana, na mengineyo mengi yawe ndio siri kubwa ya kushinda kwa kuweza kushika dola.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo amewapongeza wananchi wa Miono kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ila kubwa zaidi amewataka siku ya kupiga kura ikifika wajitokeze kwa wingi na kuyafanya yale ya kumpa kura Dr. JPM.


“Naamini Dr.Magufuli atashinda lakini kubwa zaidi ni wananchi kuona yale waliyokuwa wakiyalilia na tayari chama cha mapinduzi kimeyafanya kwa kiwango kikubwa”Alisema Kikwete

MWISHO

Post a Comment

0 Comments