SONGE AZIDI KUWA TISHIO BUSEGA.

 Na Shushu Joel,Busega

MGOMBEA Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Busega Mkoani Simiyu Simon Songe amezidi kuwa tishio kwa wapinzani kutokana na ahadi zake zake kwa wananchi wa Jimbo hilo.

 Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nyamikoma,Kata ya Kabita wilayani Busega Songe alisema kuwa ni kipindi kirefu kumekuwa na changamoto ya mafuriko katika kijiji hiki lakini kuweni pindi tu mtakaponichagua kuwa mbunge wenu changamoto hiyo inakwenda kubaki kuwa ni historia kutokana na jinsi tutakavyotengeneza miundombinu iliyo bora kwa wananchi.

Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM wilaya ya Busega Ndg.Saimon Songe akizungumza na wananchi wa Nyamikoma.(NA SHUSHU JOEL)
  

“Kunichagua mimi peke yangu haitoshi cha msingi ni kuchagua mafiga matatu ambayo ndio yatakuwa kibiko ya kupikia chakula kitanu yaani Diwani wa CCM,Mbunge wa CCM na Rais wa CCM”Alisema Songe.

Aidha aliwataka wananchi kuendelea kuwa na imani na chma cha mapinduzi(CCM) kwani ndio chama pekee chenye Ilani hapa nchini hivyo nawaombeni muachane na porojo za hawa wakosa mipango kazi kwa wananchi kwani kazi zao ni kuwatukana tu watu na sio kuomba kura kwa wananchi.

“Kumbukeni nchi hii imetolewa mbali na wazee wetu hivyo kila mmoja wetu anapaswa kuendeleza heshima tuliyoachiwa na wazee wetu”Alisema Songe.

Naye Nyabusu Mayala amempongeza mgombea ubunge Saimon Songe kwa  kusema kuwa kwa jinsi Mgombea anavyoonekana kuwa na hofu ya Mungu ni kweli wananchi tunamatumaini makubwa na kauli zake anazozisema.

 

 

 

 

 

 

 

Aliongeza kuwa mbali na kutatua changamoto za mafuriko tunakuomba nasi kina mama utuangalie kwa jicho la tatu kwa kututafutia masoko  ya mboga mboga zetu.

Kwa upande wake Diwani mstaafu wa kata hiyo Daniel Ntalima ambaye pia ni mmoja wa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya  mafuriko hayo amepongeza jinsi Songe alivyowaahidi wananchi na hasa juu ya kutatua kero ya mafuriko.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments