MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BARIADI AAHIDI KUPAUA MABOMA YA SHULE YA MSINGI GIRIKU A"

Na Bahati Sonda , Bariadi.


Mgombe ubunge jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu, kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Mhandisi Andrew Kundo amehaidi kupaua maboma yote ambayo hajapauliwa katika shule ya Msingi Giriku A ikiwa ni kuunga jitihada za serikali ya awamu ya tano ya utoaji wa elimu bure.

Mhandisi Kundo amesema kuwa mbali na kupaua maboma atahakikisha upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia ,miundombinu bora na mazingira rafiki huku akiongeza kuwa kumeuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaoandikishwa kuingia darasa la kwanza pamoja na kidato cha kwanza baada ya kuanza kwa mfumo wa elimu bure Katika shule za Msingi na sekondari.

Mgombe ubunge jimbo la Bariadi Mhandisi Andrew Kundo akizungumza na umati wa wananchi wa  Kata ya Bhunamhala , waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea huyo ambazo zinaendelea katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
 

Mgombe huyo ametoa ahahdi hiyo mbele ya umati wa wananchi wa kijiji Giriku na Mwakiboro kilichopo katika Kata ya Bhunamhala , waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea huyo ambazo zinaendelea katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

"Niwahakikishie wananchi kuwa maboma yote ambayo hajapauliwa katika shule ya Msingi Giriku A yatapauliwa na kwamba mabati yataletwa mpaka yatabaki" Alisema Kundo

Aidha Kundo aliwahakikishia wananchi kutengeneza barabara zote ambazo ambazo zimekuwa kikwazo ili ziweze kupitika kwa urahisi na kuwawezesha kuondokana na kero hiyo inayowapa adha ya kusafiri kutoka eneo moja kwenda lingine kutafuta mahitaji maalumu pamoja na kwenye shuguli za uzalishaji.

"Wakati nakuja hapa nimepitia hii Barabara nimeona jinsi ambavyo mnateseka na njia, nihaidi hapa mbele yenu, naenda kuhakikisha barabara zote zinapitika muda wote, kazi yangu itakuwa hiyo kupambana Barabara zipitike," Alisema Mhandisi Kundo.



Wakizungumzia changamoto ya barabara wananchi hao wamesema kuwa wamekuwa wakipata adha zaidi katika msimu wa mvua pindi wanapotaka kwenda kutafuta huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusafirisha mazao yao kwenda kuyauza na kumuomba mbunge hiyo iwapo atachukuliwa aweze kutatua changamoto hiyo.

Alisema kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge, atahakikisha anatumia mfuko wa mandeleo ya jimbo kutatua changamoto za Elimu na Afya, nishati ya umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa ambapo katika kijiji cha Mwakiboro alihaidi kuanzisha ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.

Katika hatua nyingine aliwaomba wananchi hao kumchagua, ikiwa pamoja na kumchagua mgombea urasi kupitia chama hicho Dkt John Pombe Magufuli, pamoja na Madiwani wa CCM ili kuweza kuwaletea maendeleo zaidi wananchi.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments