Na Omary Mngindo, Chalinze
JUMUIA ya Maimamu Jimbo la Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imeandaa dua maalumu ya kuombea Taifa likielekea kwenye Uchaguzi Mluu wa Oktoba 28.
Dua hiyo inayotaraji kufanyika Jumapili ya Oktoba 12 itafanyika katika Kijiji cha Mbwewe, Kata ta Mbwewe jimboni hapa, ambapo Masheikh kutoka maeneo mbalimbi wanataraji kuhudhulia dua hiyo, inayolenga kuomba amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.
![]() |
Baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu katika picha ya pamoja |
Hayo yameelezwa na kiongozi Mkuu wa Maimamu hao Alhaj Hamisi Nassoro, akizungumza na Waandishi wa habari mjini hapa, ambapo alisema kuwa dua hiyo maalumu imeandaliwa kwa ajili ya kuiombea taifa linaloeleka katika uchaguzi huo.
"Sisi Maimamu Jimbo la Chalinze tumeandaa dua maalumu inayolenga kuliombea taifa, wakati huu tukiwa katika kampeni za wagombea wa vyama vya siasa, tukielekea kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba 28 mwaka huu," alisema Alhaj Nassoro.
Aliongeza kwamba mpaka sasa wakati mikutano ya kampeni ikiendelea hakujaripotiwa taarifa zozote zinazoashiria uvunjifu wa amani, hali inayothibitishwa na ukomavu wa wa-Tanzania hususani wanachama na wafuasi wa vyama vya siasa.
![]() |
Picha ya pamoja ya viongozi hao. |
"Mpaka leo Oktoba 9 zikiwa zimesalia siku 18 kabla ya uchaguzu huo hakujaripotiwa taarifa zozote zinazoashiria kuvunjika kwa amani na utulivu wetu, niwaombe wa-Tanzania popote tulipo tuendelee kudumisha amani yetu, kuna maisha baada ya uchaguzi," alisema Alhaji Nassoro.
Aliongeza kuwa mbali ya kuliombea taifa likielekea kwenye uchaguzi huo, pia kikazungumzia mambo mbalimbali yanayohusiana na mustakbari wa nchi kuhusiana na amani, upendo na mshikamano, huku akiwaasa Masheikh kuendelea na utoahi wa elimu inayohusiana na dini.
"Sisi viongozi wa dini ya Kiislamu na hats wenzetu tuna jukumu kubwa la kuendelea na utoaji wa elimu kwa wananchi wetu katika masuala mbalimbali yanayohusiana na maadili mema kwa jamii, pia kuendelea kuliombea dua nchi yetu izidi kuendeleza amani, umoja, upendo na mshikamano," alimalizia Alhaj Nassoro.
MWISHO
0 Comments