MBUNGE wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu Mhe Simon Songe
ameanza kutatua changamoto za elimu katika Jimbo lake ili kuhakikisha wanafunzi
wanakuwa na sehemu nzuri za kupata elimu.
![]() |
| Mbunge wa jimbo la Busega Simon Songe Mwenye shati la mikono mirefu aliyeshika mfuko wa saruji akimkabidhi mtendaji wa kata hiyo.(PICHA NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza na baadhi ya wananchi wa
kata ya Imalamate Mbunge huyo alisema kuwa ili taifa lije kuwa na viongozi
wazuri ni vyema kama kiongozi wa watu nikawekeza katika elimu.
"Wananchi wa kata ya Imalamate wamenikosha sana kwa kuanza ujenzi wa shule ya sekondari nami kama
mbunge wao nimewaunga mkono kwa kuwachangia kiasi cha pesa shilingi laki tano na
mifuko ya saruji 60"Alisema Songe.
![]() |
| Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge Songe mara baada ya kukabidhi Saruji hiyo.(NA SHUSHU JOEL) |
Aidha Mbunge huyo aliwataka wananchi hao kuendelea kuwa wabunifu kwa kuibua miradi mbalimbali kwani kipindi hiki ofisi yangu imejipanga kuhakikisha inakuwa kimbilio la la wanabusega.
Naye Malimi Fumbuka(57) Mkazi wa Imalamate amempongeza mbunge Mhe Songe kwa jinsi
anavyojitolea kwa jamii hivyo tunaimani jimbo letu litakuwa la mfano kwenye
maendeleo.
![]() |
| Mbunge Saimon Songe sambamba na wananchi wa kata ya Imalamate wakiangalia shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu za wananchi.(NA SHUSHU JOEL) |
Kwa upande wake Masalu Manyilizu alisema kuwa upatikanaji wa bati,saruji mifuko 60 na kiasi cha laki tano kutapelekea kukamilika haraka kwa
shule yetu na hivyo matumaini makubwa kwa watoto wetu mwezi January kuanza
shule.
MWISHO



0 Comments