Na Shushu joel,Busega
MGOMBEA ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika jimbo la Busega Mkoani Simiyu Mh Simon Songe amewahakikishia wananchi wa kata ya Badugu kuwa pindi watakapomchagua kuwa Mbunge atahakikisha anawafuta machozi kwa kuwaletea maendeleo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Busami Songe alisema kuwa ni kipindi kirefu wakazi wa eneo hili wamekuwa wakisumbuliwa na changamoto za ukosekanaji wa zahanati ambapo wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kijiji jirani kupata huduma za Afya hivyo mara tu mtakapoichagua CCM ni lazima kijiji hiki kipate zahanati,pia changamoto nyingine ni barabara ya kutoka Mwanangi mpaka Busami nayo pia tutaishughulikia ili kuweza kurahisisha usafirishaji.
![]() | |||||||||||||||||||||||||
Mbunge wa Jimbo la Busega Simon Songe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Busami(NA SHUSHU JOEL) | |
Aidha Songe amewakumbusha wakazi wa eneo hilo kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili wakampigie kura Rais Dr. Magufuli,Mbunge Songe na Diwani Deus ili kutengeneza mafiga matatu ya maendeleo.
Kwa upande wake Bi,Tabu Makenanguji(48) alisema kuwa kukosekana kwa huduma ya Afya katika kijiji cha Busami ni jambo la muda mrefu lakini kutokana na ujio wa Songe tunaamini jambo hilo linakwenda kupatiwa ufumbuzi.
"Tulikuwa tukipata changamoto sana kinamama na hasa wakati wa kujifungua lakini Songe katuhakikishia lazima zahanati hiyo imaliziwe ili ianze kazi mara moja"Alisema Bi, Tabu.
![]() |
Mh Simon Songe akizungumza na wananchi wa kata ya Badugu juu ya ujio mpya wa maendeleo (NA SHUSHU JOEL) |
Naye Sostenes Sospeter amempongeza Mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi(CCM) kwa kuonyesha jinsi gani alivyo na uchungu wa kuwahudumia wananchi wake wa Jimbo la Busega.
Aidha aliongeza kuwa kwa jinsi ambavyo Mh Songe anavyojitoa inaonekana kuwa ni kiongozi mwenye hofu ya Mungu hivyo tunaamini atatufikisha mbali.
![]() |
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa mbunge Songe katika kata ya Badugu(NA SHUSHU JOEL) |
Aliongeza kuwa katika kijiji chetu hakuna wa kuwapigia kura wapinzani na atakayefanya hivyo cha moto atakiona kwani hii inatokana na kuwa CCM ina Ilani yenye kuwatumikia wanyonge.
"Mh Songe muonekano wake ni kama wa Rais Dr Magufuli kwani ni mwenye huruma,mpenda watu ,asiyependa kuona wanyonge wananyanyasika na kubwa zaidi ni mcha Mungu"Alisema.
MWISHO
0 Comments