AFISA VIJANA SINGIDA AFUNGUA NJIA ZA MAFANIKIO KWA VIJANA

Na Shushu Joel.

AFISA vijana Mkoa wa Singida  Ndg Frederick Ndahani amewataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo ndani ya kilimo kwani kuna pesa nje nje.

Afisa Vijana mkoa wa Singida akiwa shambani kwake(PICHA NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza na Waandishi wa habari walipomtembelea shambani kwake Ndahani alisema kuwa fursa katika nchi hii zipo nyingi cha msingi ni jinsi ya kuzichangamkia ili ziweze kukunufaisha. 

"Vyema sasa vijana wenzangu tukajidhatiti kwenye kilimo kwani licha ya kuwa ni uti wa mgongo pia ni  fursa ya mtu kujikwamua kiuchumi"Alisema Ndahani.


Aidha Afisa vijana huyo amewakumbusha vijana kuwa na tabia ya kusikiliza hotuba za viongozi wa kitaifa na kimataifa kwani wengi wao wamekuwa wakisisitiza kilimo kuwa ni mkombozi wa maisha, Hivyo amewataka kutokusingizia mitaji kwani siku hizi mikopo ipo mpaka mitaani.



Naye Mwajuma Iddy amempongeza Afisa vijana huyo kwa kufungua njia kwa vijana kwani ilikuwa ni ngumu kuamini lakini kumbe inawezekana  kuondokana na umasikini kupitia kilimo.


Kwa upande wake Ally Mohamed amesifu juhudi za Afisa vijana huyo na kusema ni mfano wa kuigwa.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments