WAZEE NI TUNU YA TAIFA ASEMA MBUNGE WA BUSEGA SIMON SONGE

Na Shushu Joel,Busega 

MBUNGE wa Jimbo la Busega,wilaya ya Busega   Mkoani Simiyu Mhe. Simon Songe  amewapongeza wazee kwa kuzidi kuiamini serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli  katika utendaji wake wa kazi kwa kuwajali wanyonge. 

Mbunge wa jimbo la Busega Simon Songe akiongoza kikao cha wazee wa jimbo hilo(NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza na baadhi ya wazee wa Jimbo hilo waliojitokeza kwenye kikao kazi,Songe  alisema kuwa kitu pekee ambacho serikali ya ccm  inazidi kujivunia ni kuwa na wazee wenye hekima na mapenzi ya dhati kwa chama hicho kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika jamii.


Wazee wamekuwa ni washauri wakubwa kwetu vijana juu ya chama chetu kwani unapokosea jambo wazee wanakuhita na kukukanya hivyo uwepo wao ndani ya Jimbo langu  ni fursa kwetu”Alisema Songe 

Aliongeza kuwa wazee walio ndani ya CCM wamekitoa mbali chama hiki kwani kabla ya uwepo wa ccm kulikuwepo na  Tanganyika African Association(TAA) kisha kikaja chama  cha Tanganyika African National Union(TANU) hivyo uwepo wa wazee ndani ya chama hiki ni tunu ya pekee katika taifa letu.


Nimekutana na wazee kwa lengo la kuchukua changamoto zao zinazowakabili na kwenda kuwasemea kwenyechombo cha maamuzi yaani (Bunge).

Mwalimu Mstaafu Ntale akisisitiza jambo kwa Mbunge Mh Songe


Aidha Songe alisema kuwa changamoto za wazee ni nyingi na zinahitaji kusemewa kwenye vyombo vya maamuzi ili ziweze kutatuliwa na wao waweze kunufaika na nchi yao kama ilivyokuwa wakinufaika enzi za ujana wao.


Kwa upande wake Mwalimu Jonathan  Ntale  (85) alisema kuwa wao kama wazee waliamua kumuomba Mbunge kuonana naye ili wampatie ajenda zao ambazo zitawanufaisha pindi zitakapopelekwa Bungeni na kuamuliwa na wawakilishi wa kila sehemu.

"Tumenufaika sana kukutana na kutoa mawazo yetu kwa mbunge wetu kwani ilikuwa ni ngumu kufikisha kwake lakini amekuwa ni kijana mwadilifu na mwenye kuthamini watu wa rika lote kweli Mbunge tumepata na atatufikisha pale tulipokuwa tukipahitajika kufika" Alisema Mwalimu Ntale.


Naye Bi Anima Malimi (63) alisema kuwa  Songe ni mbunge wa pekee na mwenye maono ya mbali kwa watu wa Busega katika suala la maendeleo na ufunguaji wa fursa .


Aidha amempongeza mbunge wa jimbo la Busega Simon Songe  kwa kutambua thamani ya wazee na hata kuwakutanisha wazee na kuwataka waeleze changamoto zinazowakabili na zjnazohitaji kutatuliwa na Serikali au zile zake mwenyewe kama Mbunge.


Hivyo aliongeza kuwa wao kama wazee wamejipanga ili kuhakikisha wanakuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha maendeleo ya Busega yanapatikana kwa wananchi wote.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments