RC MTAKA AFUNGUKA JINSI ANAVYOJIONGEZEA MAARIFA YA UONGOZI KWA KUSOMA VITABU

Na Shushu Joel,Bariadi

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akifafanua jambop kuhusu namna ambavyo kiongozi unaweza kuwa mbinifu wa uongozi katika usomaji wa vitabu mbalimbali(NA SHUSHU JOEL)


 Mwaka 2020 nilisoma vitabu vilivyoniongezea maarifa mapana katika maeneo ya uchumi, uongozi wenye matokeo,uelekeo wa dunia katika maeneo ya Teknolojia, ajira na ushindani katika mambo ya kijamii. Nimepata mwanga pia katika eneo pana la uthubutu kwa viongozi wa mataifa katika utumiaji wa raslimali zao kwa faida pana ya jamii zao.

 

Mwaka huu 2020 nimepata nafasi ya kuwasoma waandishi wa Kitanzania ambao wametumia uzoefu na ubobezi wao katika kuangazia raslimali za taifa letu, umahiri wa uongozi katika uchumi shindani wa kibiashara, sekta ya fedha nchini, sambamba na uibuaji wa fursa mpya za uwekezaji kwa mabenki yetu.

 

Dkt.Charles Kimei , mmoja wa Wabobezi wakubwa katika uongozi wa Mabenki Nchini hajatuacha yatima baada ya utumishi wake kwa zaidi ya miaka 40 katika benki ya CRDB na BOT. Dkt. KImei  ametuachia kitabu kizuri kilichosheheni uzoefu na weledi mkubwa kwenye sekta ya fedha na mabenki.

 

Dereck Murusuli ameziangazia fursa za Tanzania na Bara letu la Afrika na kuelezea kwa mapana umuhimu wa ushupavu wa uongozi katika kuzisimamia raslimali kiasi cha kulifanya Bara letu lenye utajiri wa kila aina ya raslimali kuweza kujitegemea kiuchumi na kuondokana na utegemezi wa mataifa ya nje.


Kiujumla upo mwamko mkubwa sana kwa watanzania kuandika vitabu vinavyogeuka kuwa chakula bora katika akili za wasomaji wake. Katika hili nirejee kumpongeza sana Rais Mstaafu wa awamu ya 3 Marehemu Benjamini Mkapa,kwa kutuachia maandishi ya kutosha kumwelezea kwa kizazi cha leo na kijacho. Mzee Mkapa alituachia mkusanyiko wa Hotuba zake zote katika kipindi cha uongozi wake kwa miaka 10, ambapo aliziweka katika vitabu vya kiswahili na Kiingereza,kama.haikutosha akaandika kitabu kilichoeleza kwa ufasaha sana wasifu wake. Nina amini hata wale ambao hawakumfahamu mstaafu Rais Mkapa,watakapopata nafasi ya kukisoma kitabu chake wataona hazina ambayo Mungu aliiweka ndani yake.


Naendelea kuwahamasisha viongozi wa makundi yote, kisiasa, dini na wafanya biashara waliofanikiwa kuandika vitabu vyao.Jamii imsome Mzee Edward Ngoyai Lowasa, Mzee Fredrick Sumaye, Mzee John Malecela,Mzee Warioba Joseph Sinde, Mzee Mizengo Kayanza Peter Pinda, Dr.Salm Ahamed Salim, Mama Anna Semamba Makinda.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments