AIJAWAI TOKEA TANGU NCHI HII KUPATA UHURU MAKUSANYO YA NAMNA HII:KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA.

 Na Shushu Joel, Dar.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inazidi kuifurahisha Serikali ya awamu ya Tano Chini ya Kamanda wa vita Dkt John Pombe Magufuli kwa kuvunja rekodi zake katika ukusanyaji wa mapato.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dotto James Akizungumza juu ya mafanikio makubwa ya ukusanyaji wa mapato na waandishi wa habari hawapo pichani(NA SHUSHU JOEL}

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisi kwake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha  Dotto James alisema kuwa Mamlaka ya Mapato nchini(TRA ) imekuwa ikijifunjia rekodi zake  kutokana na mikakati ya serikali ya Dkt Magufuli kuhitaji kulikomboa Taifa letu.


"Tangu nchi hii tupate uhuru aijawai kutokea ukusanyaji huo wa tija na wenye kulisaidia taifa katika nyanja ya ukusanyaji"Alisema James


Aliongeza kuwa kuongezeka kwa makusanyo huko kutapelekea kukamilisha kwa miradi mikubwa inayojengwa na Serikali kupitia fedha zetu za ndani ,Hivyo kukamilika kwa miradi hiyo kusaidia shughuli nyingi za kila siku na hata kurahisisha maisha ya Watanzania.


Aidha amewataka watendaji wa Mamlaka ya Mapato nchini kuendelea na utoaji wa elimu kwa wananchi ili kila mmoja ajue na kuona umuhimu wa kulipa kodi katika Taifa lake.

James Dotto Katibu Mkuu wa wizara ya fedha akifafanua jambo

"Niwapongeze kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ila msibweteke kwani nyie ndio ndio tunawaangalia kwenye ufanishaji wa miradi ya wananchi"Alisema Katibu James.


Naye Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)  Dr Edwin Mhede amewapongeza wananchi na hasa wafanyabiasha kwa uzalendo wa hali ya juu wa kuendelea kulipa kodi kwa hiyari na kwa wakati licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali.

Aidha amewashukuru walipa kodi wote waliolipa kodi zao kwa wakati na kuiwezesha mamlaka kufikia makusanyo ya shilingi Trilion 2.088 kipindi cha mwezi Desember 2020 ikilinganishwa na lengo  la kukusanya Trilion 2.072 .


MWISHO 

0717913670

Post a Comment

0 Comments