WAAMINI WA KANISA KATOLIKI MKOA WA SINGIDA NA DODOMA WALIOMBEA TAIFA.

Na Shushu Joel 

Ikiwa Leo ni Siku ya Kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika,Waamini wa kanisa Katoliki wa Majimbo ya Singida na Dodoma wamekusanyika kuaadhimisha Misa Takatifu ya Kuliombea Taifa la Tanzania,Ambapo Misa hiyo imefanyika katika Kijiji cha Sukamahela Wilayani Manyoni ambapo kijiografia ndipo katikati ya Nchi ya Tanzania.

Aidha katika eneo hilo lililotengwa na Jimbo kwa ajili ya kituo cha Hija limekuwa likitumika kwa lengo la kuombea Taifa kwa Maombezi ya Mama Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili.


Akiadhimisha Misa Takatifu Mhashamu Baba Askofu Edward Mapunda amewaomba Watanzania kuendelea Kuliombea Taifa ili liendelee kuwa na umoja ,upendo, mshikamano na Kustawi kimaendeleo zaidi,"Taifa hili lilikabidhiwa na Baba wa Taifa chini ya ulinzi na usimamizi wa Mama Bikira Maria hivyo NI wajibu wetu kuheshimu Maono ya Baba wa Taifa"Alisema.


Kwa upande wake Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ambaye ndiye Muasisi wa kituo hiki Amesema Tanzania imekuwa Nchi inayoponya Mataifa mengine toka enzi za Baba wa Taifa,Wakati wa Kudai Uhuru Mataifa mengi yalikuja Tanzania kwa lengo la kupanga namna ya kujikomboa na Ukoloni,

Hivyo Tanzania ni Taifa la uponyaji,Na kwasababu Singida ni Katikati ya Tanzania wamewaomba Wananchi na Viongozi husasani Ikulu kuwa na Amani kwa kuwa Singida imejipanga kuwalinda Kimwili na Kiroho.


Na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Dkt Pius  Chaya amemushukuru Baba Askofu kuteua eneo la Sukamahela kuwa Kituo kikubwa cha Hija ambapo kitasaidia kuinua Uchumi wa Wilaya,katika Salamu zake Mbunge amechangia Shilingi million moja kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha Ufundi Stadi.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments