Na Shushu Joel,Mkuranga
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt Festo John Dugange ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kufungua kituo cha afya Vikindu ifikapo Januari 30, 2021 ili wananchi waweze kupata huduma za afya msingi.
![]() |
Dkt Dugange akifafanua jambo mbele ya viongozi wa wilaya ya Mkuranga(NA SHUSHU JOEL) |
zilizokusudiwa ikiwa ni pamoja na huduma za kliniki za mama na mtoto, na matibabu kwa wagonjwa wa nje.
Dkt Dugange ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo baada ya kubaini kuwa mradi uliojengwa kwa fedha za Serikali ya shilingi milioni mia mbili umekamilika miezi sita iliyopita bila kutoa huduma kwa wananchi kwa maelezo kuwa wanasubiri vifaa toka bohari ya Dawa.
Aidha Dkt. Duganhe ameitaka menejimenti ya Mkuranga kujiongeza kwa kununua vifaa vya msingi vya kuanzia ili kukata kiu waliyonayo wananchi ya kuonja matunda ya mafanikio ya Serikali yao inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Awali wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri Dkt. Festo John Dugange alifanya kikao cha ndani na viongozi wa wilaya, kisha kukagua hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Mkuranga, ujenzi wa barabara ya Vikindu-Sangatini unaogharimu shilingi milioni mia nne na kusimamiwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) na kisha kuhitimisha kwa kukagua ujenzi wa stendi ya Kisasa ya mabasi Kipala-mpakani.
MWISHO
0 Comments