Julieth Ngarabali, Chalinze,
Wananchi katika Halmashauri ya Chalinze Pwani wametakiwa kuimarisha usafi wa mazingira msimu huu wa mvua ili kuwaepusha watoto wadogo chini ya miaka mitano wasidhurike na magonjwa mbalimbali ya mlipuko kwani kundi hilo hupenda kuchezea matope ,maji machafu na baadhi ya vifaa vilivyotupwa.
Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Chalinze, Betha Mchopa ametoa tahadhari hiyo wakati akieleza jitihada zinazofanyika kuhakikisha watoto hao wadogo wanakua salama msimu huu wa mvua na hata nyakati zingine
Alisema watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano hupenda kuchezea maji machafu ya mvua yanayotiririka kama sehemu yao ni michezo na kuokota vitu vinavyo safiri na maji hayo ikiwemo taulo za kike,pampasi ambayo ni hatari hivyo kuweza kusabaisha magonjwa ya kuambukiza na yale ya mlipuko
Mchopa alisema wameanza kutoa elimu kwa jamii katika maeneo mbalimbali kuhakikisha wanapotumia taulo za kike au pampas wachome ili kila familia iwe salama hasa kipindi Hilo Cha mvua
"Mara nyingi wakati wa mvua mnakuta kuna na magonjwa mengi ya kuambukiza kama matumbo yanayotokana na uchafu, tunaomba kila mtu aweke mazingira yake safi"amesema
Mmoja wa wakazi wa eneo la Chalinze Mzee Shida Kuyunga ameshauri elimu ya afya iwe inatolewa Mara kwa Mara na sio msimu wa mvua tu.
Ashrafi Mudi ameongeza kuwa ukaguzi wa nyumba kwa nyumba ufanyike ili kuwabaini wasio na mashimo ya taka au mapipa ya kutunzia taka kwani hao ndio wanasabaisha taka kusambaa na kuleta magonjwa.
Mwisho
0 Comments